Saturday, June 4, 2022

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AMEKUTANA NA UONGOZI WA JUMUIYA YA ISTIQAAMA ZANZIBAR LEO IKULU

 

VIONGOZI wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 4-6-2022, kwa kujitambulisha na kuelezea kazi za Jumuiya hiyo kwa Jamii ya Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza  Kiongozi wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar Sheikh.Sultan Khamis Mbarouk  akizungumzia changamoto za Jumuiya yao wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 4-6-2022, walipofika kujitambulisha na kuelezea kazi za Jumuiya yao kwa Jamii ya  Zanzibar.

   

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar, walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha na kuelezea Kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo kwa Jamii, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Kitabu kinachohusiana na Jumuiya ya Istiqaama, akikabidhiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Zanzibar, Sheikh.Salum Mohammed Salum, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar Sheikh.Salum Mohammed Salum, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, leo 4-6-2022, na Ujumbe wa Jumuiya hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Ujumbe wa Jumuiya ya Istiqaama Zanzibar  ukingozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh.Salum Mohammed Salum, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 4-6-2022.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment