Tuesday, June 14, 2022

MKUU WA MKOA WA TANGA AMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy na Ujumbe waliofuatana nao (hawapo pichani), walipomtembelea ofisini kwake Juni 13, 2022 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima (katikati) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy (kulia) baada ya kikao chao kilichofanyika ofisini kwake Juni 13, 2022 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Transfoma iliyofungwa katika kijiji cha Msomera, Kata ya Misima, wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga, ikiwa ni kazi iliyofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kupeleka umeme ili kuboresha miundombinu katika eneo wanalohamia wananchi wa jamii ya wafugaji kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima (katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (wa tatu-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy (wa tatu-kulia) na Ujumbe waliofuatana nao, walipomtembelea ofisini kwake Juni 13, 2022 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima (wa nne-kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (wa tatu-kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy (wa tatu kutoka kulia – mbele) na Ujumbe waliofuatana nao, walipomtembelea ofisini kwake Juni 13, 2022 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy (katikati) baada ya kikao chao kilichofanyika ofisini kwake Juni 13, 2022 wakiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

Madereva kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ibrahim Shembilu (kushoto) na Kasongo Rubeya wakifurahia jambo wakati wa ziara ya viongozi wa REA kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini mkoani Tanga, Juni 13 mwaka huu. Madereva ndiyo huwawezesha viongozi na wataalamu wa Wakala kufika sehemu mbalimbali za kazi ili kutekeleza majukumu yao.

Na Veronica Simba  – REA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Adam Malima amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha utekelezaji wenye ufanisi wa miradi ya umeme vijijini.

Alitoa pongezi hizo Juni 13 mwaka huu, wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy waliomtembelea ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kazi mkoani humo.

“Sisi tuna bahati kwani hakuna Wilaya iliyokosa Mradi wa REA. Tuna kila sababu ya kuishukuru Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Nishati, REA pamoja na TANESCO,” alisema Mkuu wa Mkoa.

Akieleza zaidi, Mheshimiwa Malima alisema anaipongeza REA kwa kazi kubwa inayofanya kusambaza umeme vijijini nchi nzima. Alisema REA imefanya kazi ambayo ni mfano kwa Afrika nzima na kwamba  ziko Taasisi zinazotamani kuja kujifunza kutoka kwao.

Akizungumzia miradi inayotekelezwa na REA, Mkuu wa Mkoa alibainisha kuwa ni miradi inayogharimu mabilioni ya fedha ikiwa ni uwekezaji ambao Serikali inafanya kwa lengo la kuwanufaisha wananchi wake na siyo kujipatia faida.

Alisema kuwa wananchi wa Tanga wanajielewa na wamejipanga kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kwani wanatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na Serikali kuwapelekea nishati hiyo kwa gharama nafuu ya shilingi elfu 27 tu.

Aidha, alikemea tabia inayofanywa na baadhi ya watu kuiba au kuharibu miundombinu mbalimbali iliyowekwa na Serikali kwa gharama kubwa ikiwemo ya umeme.

Aliahidi kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa italishughulikia suala hilo kwa kuliweka miongoni mwa ajenda maalumu na kwamba yeyote atakayebainika kuhujumu miundombinu husika, atachukuliwa hatua za kisheria.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Malima aliipongeza REA kwa kutafuta ufumbuzi wa masuala ya nishati inayotumika kupikia katika maeneo mbalimbali.

Akifafanua, alisema kuwa matumizi ya mkaa yamekuwa na athari hasi kwenye Mkoa wa Tanga ambapo yamesababisha uhaba wa maji yanayotiririka kutoka milimani kiasi cha kuathiri vituo vya kuzalisha umeme vya Hale na Pangani.

Alisema kuwa, kufuatia hali hiyo, Mkoa wa Tanga unaandaa Mkakati wa kupanda miti itakayotumika mahsusi kama kuni za kupikia na kuiomba REA ichangie ufadhili wa kampeni hiyo kutoka katika bajeti yake.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Kalolo alimshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuiwezesha REA kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha, Wakili Kalolo alishukuru ushirikiano ambao REA inaupata kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wakuu wa Wilaya, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa ngazi mbalimbali mkoani humo katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.

Awali, akitoa taarifa ya ziara husika kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa REA Mhandisi Saidy alibainisha kuwa kwa sasa Wakala unalenga kujikita pia kwenye kufikisha nishati ya kupikia kwa wananchi.

“Tumeanza na kusambaza gesi Mkoa wa Lindi na Pwani, lakini tunataka pia tupanue huduma zetu, tuangalie zaidi ya gesi ni nishati gani nyingine inaweza kutumika kwenye shughuli za kupikia,” alifafanua.

Viongozi hao wa REA wako katika ziara ya siku tatu mkoani Tanga, inayolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini.

No comments:

Post a Comment