Mwenyekiti wa Kampeni ya shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii SMAUJATA kwa mkoa wa Singida Bw. Vicent Mafuru , wa pili kulia akiwa ameambatana na Kaimu Mwenyekiti Bi Ambwene Kajula wa pili kutoka kushoto na baadhi ya viongozi wa Baraza la Wazee la Mkoa wa Singida wakiwa katika ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii Mkoani Singida kuzungumzia mikakati ya kupambana na ukatili katika jamii.
Afisa Ustawi wa jamii mkoani Singida Bi. Felician Mboya akizungumza katika kikao na SMAUJATA
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Singida Yustina Ngaiza akisikiliza jinisi mikakati ya SMAUJATA itakavyo simamia suala la kupinga ukatili kwa mkoa wa Singida.
Mazungumzo yakiendelea ofisi ya afisa Ustawi wa Jamii ya mkoa wa Singida.
Mwenyekiti wa SMAUJATA kwa mkoa wa Singida Bwana Vicent Mafuru akizungumza jambo kwenye kikao hicho.
Mazungumzo yakiendelea ofisi ya afisa Ustawi wa Jamii ya mkoa wa Singida.
Katibu wa Baraza la wazee mkoa wa Singida Mzee Ramadhan Tuji akisikiliza mazungumzo ya SMAUJATA.
Na Hamis Hussein - SINGIDA
Kampeni
ya shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamii Tanzania SMAUJATA kwa mkoa wa Singida
imedhamilia kuwafikiwa wananchi kutoka katikka maeneo mbalimbali hasa
kwa wale wanaoishi maeneo ya vijini ili kuwapa elimu ya namna
kupinga na kuufuta kabisa ukatili na unyanyasaji unaoikumba jamii hapa nchini.
Akizungumzia
mikakati ya SMAUJATA mkoani Singida katika utekelezaji wa kampeni hiyo iliyo
chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsi, wanawake na Makundi maaalum Bw. Vicent
Mafuru amesema kuwa wao kama
wanaharakati wataufikia mkoa wa Singida kuanzia ngazi ya Halmshauri , kata
,vitongoji hadi vijiji na mitaa ili kutoa elimu na misaada mbalimbali ya namna
ya kukabiliana ukatili wa kijinsi ili kulifanya taifa la Tanzania kuwa endelevu
katika Nyanja zote za kijamiii na kiuchumi.
Mafuru
alisema Jamiii mkoani hapa inatakiwa kutoa taarifa zinazohusu ukatili dhidi yao
hasa wakati huu wa utekelezaji wa
kampeni ya kupinga ukatilii ijulikanayo Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamiii
Tanzania SMAUJATA .
“Wanajamiii wanatakiwa
kutoa taarifa za matendo maovu yanayoendelea katika nyumba zao, shuleni na maeneo yote ambayo watu
wanakumbana na kaadhia ya unyanyasaji na ukatili kwa kupiga namba 116 na
atapata msaada, Pia watu wajitolee katika kufanikisha kampeni hii, kampeni
ambayo tunatakiwa kuona tumeumia na kunyanysika vya kutosha na kufikia hatua ya
kuwa lazima tukatae unyanyasaji”
Alisema Mafuru Mwenyekiti wa SMAUJATA Singida.
Aliongeza
kuwa ofisi ya afisa ustawi wa jamii mkoani Singida imewaelekeza wanaharakati
hao kufika hadi ngazi za halmashauri na
vijiji kutoa elimu ya kuukomesha ukatili katika jamii ambapo pamoja na mambo
mengine alishukuru uwepo wa baraza la wazee la mkoa kwani litawasaidia katika
kupata mwongozo wa namna ya kuifiki
jamii katika kufanikisha lengo la
SMAUJATA.
“Nashukuru kuwa
tutafanya kazi pamoja nanyi wezee wetu ambao mnauzoefu katika utetezi wa haki za wazee na naamini siyo kwa wazee tuu
pia mtatuongoza pia hata katika makundi mengine ili kutokomeza ukatili” Mafuru alisema.
Makamu
mwenyekiti wa SMAUJATA mkoani Hapa Ambwene Kajula alisema kampeni hii ya shujaa
wa maendele na ustawi wa jamiii Tanzania imekuja wakati mwafaka kwani makundi
mengi yanakumbana na ukatili lakini
yanaogopa kutoa taarifa ikiwemo kundi la watoto , wazee ambao mara nyingine
hukatiliwa kutokana na imani potofu kama kuhisiwa na ushirikina , lakini pia
kuna wanaume ambao hupigwa na wake zao lakini wamekuwa hawasemi, hivyo basi
kupitia kampeni hii tukishirikiana itakuwa msaada mkubwa sana.
Afisa
Ustawi wa jamii Mkoani Singida Bi. Felician Mboya baaada ya kusikiliza mikakati ya SMAUJATA kwa
aliwaelekeza wanaharakati hao kushirikiana na Halmshauri na vijiji katika kutoa
elimu dhidi ya ukatili na unyanyasaji
katika jamii na kuitaka timu hiyo
kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo maadhimisho ya siku ya
kupinga ukatili dhidi ya wazee inayotarajiwa kufanyika June 15.
Timu
hiyo ya SMAUJATA kwa hapa Singida ilikutana na baadhi ya viongozi wa baraza la
wazee la mkoa katika ofisi za afisa ustawi wa jamii ambapo wamekubaliana
kushirikiana katika suala zima la
kampeni hiyo ambapo kwa niaba ya baraza la wazee ,Ramadhan Tuji katibu wa
baraza aliishukuru Serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia,
wanawake na makundi maalum kwa kuanzisha kampeni .
No comments:
Post a Comment