Monday, May 9, 2022

WANANCHI WA KIJIJI CHA MAHENGE KUNUFAIKA NA MRADI WA TFCG

Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa wilaya ya Kilolo juu ya umuhimu wa msitu wa asili wa Mahenge ambao umehifdhiwa na serikali ya kijiji kwa ushirikiano wa serikali ya wilaya na mkoa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akipata maelezo kutoka kwa wataalam wa wilaya ya Kilolo juu ya umuhimu wa msitu wa asili wa Mahenge ambao umehifdhiwa na serikali ya kijiji kwa ushirikiano wa serikali ya wilaya na mkoa

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

WANANCHI wa kijiji cha Mahenge wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wanatarajia kunufaika na mradi wa uvunaji wa mbao na uchomaji wa mkaa kwa kutumia miti ya asili iliyopo katika msitu  wa asili uliohifadhiwa wa Mahenge.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo alisema kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha wananchi wanaouzungunguka msitu huo wananufaika na maliasili zilizomo ndani ya msimu na kuendelea kuhifadhi msitu huo.

Lyimo alisema kuwa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi Misitu Tanzania (Mjumita), Shirika la Kuendeleza Nishati Asili Tanzania (TaTEDO) ambayo yanatekeleza Mradi wa Kuleta Mageuzi Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC) wameshatoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha mahenge juu ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu.

Alisema kuwa wameshatoa elimu ya usiamamizi wa misitu na ushirikiano baina ya wananchi na serikali katika uhifadhi na uvunaji wa maliasili zilizopo kwenye msitu huo kwa ajili ya faida za wananchi na serikali kwa ujumla.

Lyimo alisema kuwa kwa kutumia rasilimamli zilizopo kwa katika msitu wa asili wa Mahenge zinaweza kuleta maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho bila kuathiri mabadilio ya tabia nchi kwa kukata miti hovyo.

Alisema kuwa msitu huo unakadiliwa kuwa na hekari 91917 ambao unamaliasili kama miti ya asili kama miombo,wanyama mbalimbali,maeneo ya utalii na kilimo ambayo yote hayo yakitumiwa vizuri yatakuza uchumi wa wananchi na kuleta maendeleo kwa wananchi wote wa kijiji cha Mahenge.

Kwa upande wake meneja mradi wa TFCG ,Charles Leornad  alisema kuwa mradi huo utafikia ukomo ifikapo mwezi wa kumi na moja mwaka 2022 kulinga namktaba wa mradi huo ulivyo.

Leornad alisema kuwa wameshatoa elimu ya usimamizi,utambuzi wa vitalo ambavyo vinatakiwa kuvunwa na wanauhakika hata mradi ukifikia ukomo wananchi wataendelea kuvuna na kuutunza msitu huo kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae.

Alisema kuwa wanaiomba serikali kuendelea kuwasimamia na kutoa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa misitu ya asili ambavyo itasaidia katika maendeleo ya kijiji cha Mahenge na taifa kwa ujumla kwa kuwa wananchi watakuwa wanajua madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.

Leornad alisema kuwa msitu wa asili wa Mahenge unafaa kwa utalii kwa kuwa unavivutio vingi ambavyo bado watalii wengi hawajavitembelea hivyo ni wajibu wa wadau na serikali kuzitangaza vivutio hivyo kwa watalii wa ndani nanje ya nchi.

Alisema kuwa kwenye msitu wa asili wa Mahenge kuwa viti mingi ambayo inasadikika kutumiwa kama dawa za asili hivyo watafiti wengi wameombwa kufika katika msitu huo na kufanya utafiti wa miti hiyo ya dawa na watafiti wa madini nao wanatakiwa kufika katika msitu huo.

Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga  aliwataka wananchi wa kijiji cha Mahenge kuendelea kuutunza msitu huo wa asili ambao umesheni vitu vingi vyenye faida kwa taifa la Tanzania na dunia kwa ujumla.

Sendiga alisema kuwa lengo la serikali ya mkoa wa Iringa ni kuendelea kuutunza misitu yote ya asili ilivyo katika mkoa huo kwa lengo la kuendelea kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa na madhara makubwa kwa wananchi.

Alisema kuwa serikali ya mkoa wa Iringa itaendelea kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa wa Iringa.

Sendiga aliwataka wataalamu wa mkoa wa Iringa kubainisha misitu yote ya asili iliyopo na vivutio vyake vilivyopo kwenye misitu hiyo ili kuweza kuyatangaza kwa wawekezaji na watalii mbalimbali wanapofika mkoa huo kuweza kupata taarifa za misitu nafaida zake.

No comments:

Post a Comment