Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na wabunge vinara wa malezi na makuzi ya Mtoto wakati wa Semina ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA), Masuala ya uwezeshaji Wanawake katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa pamoja na Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto MMMAM, Jijini Dodoma Leo tarehe 28 Mei, 2022.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi katika jukwaa la kizazi chenye usawa, GEF Angellah Kairuki akifafanua jambo wakati wa Semina kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA), Masuala ya uwezeshaji Wanawake katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa pamoja na Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto MMMAM, Jijini Dodoma Leo tarehe 28 Mei, 2022.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Aloyce Kamamba akizungumza wakati wa Semina ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA), Masuala ya uwezeshaji Wanawake katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa pamoja na Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto MMMAM, Jijini Dodoma Leo tarehe 28 Mei, 2022.
Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo Mtoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku akiwasilisha mada kuhusu Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa Semina ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA), Masuala ya uwezeshaji Wanawake katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa pamoja na Programu hiyo, Jijini Dodoma Leo tarehe 28 Mei, 2022.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia matukio wakati wa Semina ya utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto(MTAKUWWA), Masuala ya uwezeshaji Wanawake katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa pamoja na Programu jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto MMMAM, Jijini Dodoma Leo tarehe 28 Mei, 2022.
Na WMJJWM, Dodoma
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wameeleza kusikitishwa na ukatili unaendelea katika, hivyo kupendekeza Jamii iibuke na njia za kukomesha vitendo hivyo kwa lengo la kuwa na kizazi chenye ustawi.
Kauli za wabunge zimetolewa wakati wa semina ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), utekelezaji wa masuala ya Jinsia na uwezeshaji Wanawake kupitia jukwaa la kizazi chenye usawa pamoja a programu jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto iliyotolewa kwa baadhi ya Wabunge Jijini Dodoma.
Wamesema Jamii imeelemewa na vitendo vya ukatili hivyo ni muhimu ikajengewa uwezo wa kuwakinga na kuwalinda watoto ili kuepukana na vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwafundisha watoto namna ya kujilinda wenyewe.
Akizungumza wakati wa kufungua Semina hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewaomba wabunge kuhamasisha Jamii na kuijengea uelewa na namna ya kuwalinda watoto na makundi mengine wakiwemo wanawake ambao wamekuwa wakikabiliwa na ukatili wa kila aina.
Amesema wakati awamu ya kwanza ya MTAKUWWA ikikaribia ukingoni, kuna mafanikio kadhaa yamepatikana lakini Jamii bado imesongwa na ukatili katika makundi mbalimbali hivyo, Wabunge wanaweza kusaidia kwa kuelimisha jamii kuhusu madhara ya vitendo hivyo.
Amesema baada ya awamu ya kwanza ya MTAKUWWA kufikia ukomo mwezi Juni 2022, Wizara itafanya tathmini ya Mpango huo ili kubaini mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji kwa kipindi cha miaka mitano na changamoto zilizoathiri kufikiwa.
“Tathmini inatarajiwa kubainisha masuala ya kuigwa na kutoa mapendekezo ya namna bora zaidi ya kukabiliana na changamoto na upungufu uliobainika” Amesema Mhe. Gwajima
Vilevile Waziri Dkt. Gwajima ameeeleza kwamba, Wizara inaendelea kuratibu programu ya utekelezaji wa ahadi za nchi Katika kutekeleza malengo ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa, GEF ambayo ipo katika hatua ya ukamilishwaji ili iweze kuzinduliwa mwezi Juni 2022 na kuwaomba Wabunge, wahamasishe Wananchi wajue utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Kizazi Chenye Usawa hususan katika eneo la haki za kiuchumi kwa wanawake.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Marndeleo ya Jamii, Mhe. Aloyce Kamamba ameipongeza Wizara kwa semina hiyo kwa wabunge ambayo imewanufaisha kwa mambo mengi na kuitaka Wizara kufanyia kazi maoni yaliyotolewa.
“Ushauri uliotolewa na wabunge tuufanyie kazi, suala la kutengeneza kizazi chenye usawa na huduma muhimu, mambo mbalimbali yanaangaliwa ikiwemo haki za kiuchumi, sheria, utengenezwe utaratibu mzuri utakaosaidia haya yote yashuke hadi ngazi ya jamii” Amesema Kamamba.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya ushauri kuhusu utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa Angellah Kairuki amesema Masuala ya Jamii yanamuhusu kila mmoja hivyo jamii ina kila sababu ya kukememea ukatili unaoendelea
“Kuna baadhi ya nchi ambazo zimejitokeza kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa programu hii itakayozinduliwa mwezi Juni, Wabunge programu hii ni yenu na itashuka hadi ngazi ya chini, tunaomba ushirikiano” amesema Kairuki
Baadhi ya Wabunge wakichangia mada zilizowasilishwa wameipongeza Wizara kwa hatua zinazochukuliwa katika kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa ikiwemo uanzishwaji wa programu mbalimbali.
Wakati wa Semina hiyo, mada nne zimewasilishwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Mada zilizowasilishwa ni Utekelezaji wa Mpangokazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ( MTAKUWWA), Masuala ya Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake kupitia Kizazi chenye Usawa GEF, Program ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto pamoja Huduma za Ustawi wa Jamii Nchini.
No comments:
Post a Comment