Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akimsikiliza Mkuu wa kiwanda cha PRESS A Bw.John Kaswalala (Kulia) Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Press A Magogoni Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei 2022.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Prof.Adolf Mkenda akikagua mfumo wa usomaji wa vitabu kwa njia ya mtandao unaoratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania mara baada ya kufanya ziara ya kikazi Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei 2022.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha uchapaji wa vitabu cha Press A na Press B Jijini Dar es Salaam tarehe 14 MEi 2022.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda akiangalia namna uchapishaji wa vitabu vya uono hafifu ukifanyika mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha uchapaji wa vitabu cha Press A na Press B Jijini Dar es Salaam tarehe 14 MEi 2022.
Na Mathias Canal, Dar
es salaam
Serikali imeitaka Taasisi ya Elimu Tanzania
(TET) kuweka mkakati wa ndani ya mwaka mmoja kuhakikisha inapata mashine kubwa
ya kuchapa na kutafuta tenda nafuu ya malighafi ya karatasi.
Agizo hilo linakuja wakati ambapo matumizi ya serikali kwa ajili
ya kuchapisha vitabu vya nukta nundu vinavyotumiwa na wanafunzi wasioona na
wenye uoni hafifu ikiwa ni Bilioni 15 kwa mwaka.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof.
Adolf Mkenda ametoa rai hiyo alipofanya ziara ya kutembelea vituo vya
kuchapisha vitabu cha Press A Magogoni na Press B kilichopo shule ya Uhuru
Mchanganyiko Jijini Dar es Salaam jana tarehe 15 Mei 2022 na kusisitiza kuwa
kiasi hicho kinatokana na malighafi ya karatasi inayotumika kuchapa kununuliwa
Dubai na Marekani.
“Dubai ni Jangwani, hakuna miti wakati
hawazalishi karatasi, sisi tunaenda kuchapa huko kwa fedha nyingi, nataka na
sisi tukanunue malighafi huko wanakonunua wao tuchapishe wenyewe. ”Amekaririwa
Waziri Mkenda na kuongeza kuwa
“Wafadhili
wanaotupatia fedha kwa sasa masharti ni lazima tenda ya kuchapa itangazwe
kimataifa, sasa badala sisi tutangaze tenda ya kuchapiwa bora tutangaze tenda
ya kupata mashine kubwa ya kisasa hii itapunguza gharama.”
Prof Mkenda amesema kuwa mashine kubwa zaidi
ya uchapaji huuzwa shilingi Bilioni 30, hivyo mazungumzo yanapaswa kufanyika na
wafadhili ili waweze kufanikisha hilo, kwani wanatekeleza manunuzi ya kimataifa
ikiwa ni moja ya sharti la wafadhili hao.
Waziri
Mkenda ameongeza kuwa serikali imedhamiria kuimarisha uchapishaji kwa
kuiwezesha TET kupata karatasi kwa bei nafuu, umeme wa uhakika na mashine kubwa
ya kisasa ya uchapaji kwani kupitia fedha za Mapambano dhidi ya UVICO 19
zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
imewezesha TET kuchapa vitabu vya nukta nundu vyote vya kidato cha kwanza hadi
cha sita.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)
Dkt. Aneth Komba amesema taasisi yake imepokea maelekezo ya serikali na inaanza
kuyafanyia kazi kwa haraka.
Akielezea sababu za vitabu kutochapishwa
nchini ni kutokana na gharama kubwa ya karatasi, kutokuwepo kwa umeme wa uhakika
na wa bei nafuu na mitambo ya kutosha kumudu uchapaji kulingana na mahitaji.
Amesema
Kiwanda cha uchapaji cha Press A Magogoni ni moja kati ya viwanda saba vya
taasisi hiyo na walikabidhiwa na wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tangu
mwaka 2019.
“Kiwanda
hiki kinatumika kuchapa muongozo wa walimu darasa la awali hadi la saba na kwa
mwaka huchapa vitabu milioni tatu ukihusisha na vya wenye uoni hafifu ambapo
hata hivyo mahitaji ya vitabu hivyo yanakidhi ambapo kwa wanafunzi wenye uoni
hafifu wanatumia wastani wa vitabu vitatu kwa mwanafunzi mmoja.
Katika kuimarisha ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu serikali imeandika na kuchapa nakala 57,756 za vitabu vya Kiada, Kidato cha 1 - 4 vya maandishi yaliyokuzwa kwa masomo ya Biology, Physics, Chemistry, Mathematics, Agriculture, Home Econonics, Kiswahili, Civics, Information and Computer Studies, Geography, History na English.
Aidha, imeandika, kuchapa na kusambaza vitabu vya nuktanundu nakala 9,178 kwa masomo hayo ya sekondari kwa ajili ya wanafunzi 353 wasioona.
MWISHO
No comments:
Post a Comment