Wednesday, May 18, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA BARABARA YA TABORA-KOGA-MPANDA KM 342.9,SIKONGE MKOANI TABORA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi katika Sherehe za ufunguzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 km zilizofanyika Sikonge Mkoani Tabora 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Patricia Laverley wakifungua rasmi barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 km Sikonge Mkoani Tabora tarehe 18 Mei, 2022.Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora Mzee Hassan Mwakasubi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Patricia Laverley wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 km uliofanyika Sikonge Mkoani Tabora tarehe 18 Mei, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tabora Mzee Hassan Mwakasubi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Tabora Mpanda katika eneo la Sikonge mara baada ya kuifungua barabara hiyo, wa kwanza kulia ni Meneja Mkaazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB nchini Tanzania Dkt. Patricia Laverley

       

Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Sikonge mkoani Tabora wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwahutubia katika Sherehe za ufunguzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 km uliofanyika Sikonge Mkoani Tabora 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Mzee Hassan Mwakasubi pamoja na Viongozi Wengine mara baada ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda 342.9 km uliofanyika Sikonge Mkoani Tabora

No comments:

Post a Comment