Saturday, May 28, 2022

PSPTB YAWATAKA WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA RASILIMALIWATU KUAJIRI WATAALAM WENYE SIFA






Na Okuly Julius Dodoma

Wakuu wa idara za utawala na Rasilimali Watu katika utumishi wa umma wametakiwa kuhakikisha wanaajiri wataalam wenye sifa na waliosajiliwa katika bodi ya ununuzi na ugavi ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu watumishi kushiriki mafunzo endelevu ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma kutoka Bodi ya wataalam wa ununuzi na ugavi (PSPTB) Bwn. AMOS KAZINZA wakati akiwakilisha mada kuhusu miongozo inayosimamia ununuzi na ugavi Serikalini katika kikao kazi cha wakuu wa Idara za utawala na rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Mei 27,2022 jijini Dodoma.

Amewataka maafisa hao kuhakikisha watumishi wao katika eneo la ununuzi na ugavi wanashiriki mafunzo endelelevu yanayoandaliwa na Bodi ya hiyo ili kujiongezea uwezo katika eneo la taaluma ya ununuzi na ugavi

Pia Bw. KAZINZA amesisitiza suala la ushirikishwaji wa bodi ya Wataalamu katika mashauriano mbalimbali ili kusaidia katika kutatua changamoto na wakibaini kuwa mtaalam kafanya makosa basi bodi ina dhamana ya kutoa adhabu kwa muhusika ikiwemo kushushwa daraja jambo ambalo litamsababishia kukosa sifa ya kuwa mkuu wa kitengo kokote katika eneo la ununuzi na ugavi.

"Tunajua mna mashauri mengi sana katika ofisi zenu mengine yamewashinda ila bado mnakaa nayo tunawaomba mtushirikishe ili tuwasaidia kitaalamu kutatua changamoto hizo maana sisi kama bodi ya wataalamu tunadeal na masuala yahusuyo nidhamu hivyo kwa yeyote atakayebainika kukiuka taaluma hii ya ununuzi na ugavi tutamshughulikia"Amesema KAZINZA

No comments:

Post a Comment