Saturday, April 30, 2022

WIZARA YA UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA YAIPONGEZA SUA KWA TAFITI ZAKE

  Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe akifungua Warsha hiyo

 Kiongozi wa Mradi huo wa  TRADE HUB nchini Tanzania Prof. Reuben Kadigi akizungumza na wadau lengo la warsha hiyo.

Mhadhiri Muandamizi wa Uchumi Kilimo na Masoko Dk. Fulgence Mishili akitoa  salamu kwa niaba ya Makamu Mkuu wa Chuo.

1.     Mtafiti kutoka SUA Dk. Charles Mgeni akizungumza neno la shukrani kwa mgeni rasmi kwaniaba ya Rasi wa Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara Kilimo.Joseph Kangile Mtafiti wa Mazao ya Kahawa, Sukari na Soya akitoa wasilisho kwa wadau kusuhu matokeo ya awali katika zao la kahawa.

Wadau waliojitokeza  wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti.
Wadau waliojitokeza  wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti.

 Wadau waliojitokeza  wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti.


Wadau waliojitokeza  wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti.

Mawasilisho yakitolewa.

Wwadau wakifatilia mawasilisho tofauti tofauti. 

 Amina Hezron na Calvin Gwabara, Dodoma.

SERIKALI kupitia Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara imekipongeza na kukishukuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwanamna ambavyo kinafanya tafiti ambazo zinalenga kuinua maendeleo ya Watanzania kwakufungamanisha maswala mbalimbali  yanayolenga kuboresha uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa.

Akizungumza kwenye warsha ya wadau wa mradi wa Biashara Maendeleo na Mazingira Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara mhe. Exaud Kigahe amesema kuwa mradi huo unatekelezwa katika kipindi muafaka ambacho serikali inasisitiza uwekezaji kupitia sera ya nchi ya kuinua uchumi kupitia uwekezaji katika sekta ya viwanda na biashara.

“Imani yangu kuwa kwakipindi hiki cha miaka mitano ambayo mradi huu utatekelezwa utasaidia sana kufungamanisha shughuri za biashara za bidhaa za kilimo Wanyama pori na sekta nyingine ili kuhakikisha kuwa biashara ya mazao haya yanakuwa kichocheo chaukuaji wa uchumi ambao tunasema uwe shirikishi ili kupunguza umaskini na kuleta maendeleo endelevu”, alisema Mhe Kigahe.

Akizungumzia dhumuni la warsha hiyo Kiongozi wa Mradi wa huo wa  TRADE HUB nchini Tanzania Prof. Reuben Kadigi amesema kuwa ni kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wa mradi huo wa kile ambacho kimeshapatikana kwa muda mfupi kwa utafiti wa awali .

“Mradi unatafiti athari za biashara kwa ulimwengu na watu gharama na manufaa tutumie rasilimali tulizonazo kuleta maendeleo ambapo tukitumia bila mpangilio mzuri inawezekana uwendelevu usiwepo tutakuwa tumeharibu uhalisia” alisema Prof. Kadigi.

Prof. Kadigi ameeleza kuwa mradi huo unatekelezwa ili kusaidia kubaini suluhu za kupunguza athari hasi  na kuimarisha manufaa sawa kuweza kuweka bayana hatari za biashara zinazotokana na  desturi au vitendo vya kimazoea ambavyo si endelevu kijamii na kimazingira pia .

 

“Jukumu letu kama mradi kushughurikia changamoto ngumu ya jinsi ya kuondoa athari mbaya kwa jamii na mazingira zinazosababishwa na biashara tufanye biashara ambayo itatusaidia kutuendeleza kuleta maendeleo lakini pia kuzingatia  madhara kwenye uhalisia wa mazingira “, alisema Prof Kadigi.

Prof. Kadigi amesema  lengo la mradi huo  ni kuhakikisha biashara ya mazao ya kilimo na Wanyamapori inakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi shirikishi kupunguza umasikini na moja ya njia ya utekelezaji wa maendeleo endelevu kama inavyotajwa na Maendeleo Endelevu bila kuchangia zaidi uharibifu wa mazingira na upotevu wa viumbe hai huku ukiwa umelenga kufanyia katika sekta ndogo za Sukari,Soya Kahawa, Nyama pori na Wanyamapori.

Kiongozi wa Mradi amesema mradi huo ni  wa miaka mitano umeanza mwaka 2019 na utakamilika mwezi machi Mwaka 2024 na unatekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kwakushirikiana na washirika kutoka nchi 15 tofauti za Afrika, Asia Uingereza na Brazil.

Akizungumza kwaniaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Mhadhiri Muandamizi wa Uchumi Kilimo na Masoko Dk.Fulgence Mishili amesema Chuo kikuu cha Sokoine kitaendelea kuhakikisha kitafanya tafiti na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa jamii na taifa ili kuiwezesha serikali kufanya maamuzi sahihi kupitia matokeo ya tafiti za kisayansi.

Amewashukuru wadau wote waliojitokeza katika warsha hiyo kwakutenga muda na kushiriki katika tukio hilo muhimu na kuwataka kusikiliza kwa makini matoke ohayo ya awali ya tafiti tano zilizofanywa na waweke mapendekezo na ushauri wa kina kama kuna mambo ambayo yamesahaulika kwenye matoke ohayo ya awali.

Akizungumza kwaniaba ya Rasi wa Ndaki ya Uchumi na Stadi za Biashara Kilimo Mtafiti kutoka SUA Dk. Charles Mgeni ametoa shukrani kwa Mhe. Kihage kwa hotuba ambayo amesheheni nasaha zenye kujenga na kuleta matumaini katika juhudi za kuwafikisha kuwa biashara na bidhaa za mazao ya kilimo pamoja na wanyamapori inakuwa engine ya ukuaji jumuishi wa kiuchumi na kupunguza umasikini.

“Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kitanendelea kushirikiana na serikali kutafuta ufumbuzi na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili biashara ya bidhaa ya kilimo pamoja na ya wanayamapori  hapa nchini lengo ni kuboresha sera za kibiashara na uchumi ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi wetu wanaojishughulisha na shughuri hizi”, alisema Dk. Mgeni.

No comments:

Post a Comment