Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford katika viwanja vya shule ya msingi Mkoani ambapo mpango wa elimu wa ‘Shule Bora’ umezinduliwa
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akiangalia baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na watoto wa Shule ya Msingi Mkoani kabla ya uzinduzi wa mopango wa elimu wa ‘Shule Bora’
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford wakizindua mpango wa elimu wa ‘Shule Bora’
Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibian Mhe. Vicky Ford akiongea na wageni (hawapo pichani) baada ya uzinduzi wa mpango wa ‘Shule Bora’
Na Mwandishi wetu, Dar
WAZIRI
wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa
vya Karibian Mhe. Vicky Ford amezindua mpango wa elimu unaojulikana kama ‘Shule
Bora’ Kibaha mkoani Pwani.
Mhe. Ford alisema mpango wa ‘Shule Bora’
utasaidia kuboresha elimu nchini Tanzania na utawasaidia zaidi ya watoto
milioni nne, ambapo nusu yao watakuwa ni watoto wa kike.
“Elimu ni kipaumbele kwa Rais Samia
pamoja na Waziri wa Mkuu wa Serikali ya Uingereza….ni lengo la Serikali ya
Uingereza kuisaidia watoto zaidi ya milioni 15 hapa Tanzania kupata elimu,
lakini tumeanza na hawa wachache lakini pia tumezingatia usawa wa kijinsia
ambapo nusu ya sehemu ya msaada huu utamnufaisha mtoto wa kike,”
alisema Mhe. Ford.
Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Prof. Adolf Mkenda alisema kuwa msaada wa pound milioni 180 zilizotolewa na
Serikali ya Uingereza utasaidi sana kuboresha sekta ya elimu nchini kupitia
mpango wa elimu wa ‘Shule Bora’.
Prof. Mkenda alisema pamoja na mambo mengine,
kuwa msaada wa Serikali ya Uingereza kupitia mpango huu wa elimu utasaidia sana
kuboresha mazingira ya elimu nchini ikiwa ni pamoja nan miundombinu ya shule,
vitabu na sheria pamoja na mitaala inayotumika kufundishia.
“………….
‘Shule Bora’ itaiwezesha Serikali yetu kufanya mapitio ya Sera ya elimu ya
1978, kuboresha Sheria ya Elimu, kuboresha mitaala ya elimu, kuangalia idadi ya
walimu pamoja na wakufunzi na wahadhiri,” alisema Prof. Mkenda
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Rais – Tamisemi,
Mhe. David Silinde alimhakikishia Waziri Ford kuwa fedha zote za mpango wa
elimu wa ‘Shule Bora’ zitatumika kama ilivyokusudiwa ili kuwawezesha watoto wa
kitanzania kunufaika na elimu.
No comments:
Post a Comment