Monday, April 11, 2022

WANAWAKE WA KIISLAM WAOMBWA KUTENDA MATENDO MEMA KATIKA JAMII-Mhe. MWANAHAMISI















Wanawake wa kiislamu wameombwa kutenda matendo mema katika jamii ili kuukuza uislam huku wakiaswa mambo mema wanayoyafanya ndani ya mwezi wa Ramadhani kuendelea kuyafanya katika miezi mengine ili kuufanya uislamu kuwa mfano katika jamii.

Rai hiyo imetolewa jijini dodoma na mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe.MWANAHAMISI MUNKUNDA kwenye kongamano la wanawake wa kiislamu lilofanyika jijini Dodoma masjid ghadaf lenye lengo la kuukuza uislamu na ujenzi bora wa akhera kwa waislam liloandaliwa na Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam JAI Dodoma.

Aidha MWANAHAMISI MUNKUNDA amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo ya JAI ili kuirahisishia taasisi hiyo ya JAI kuweza kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma mbalimbali katika jamii.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. FATMA TOUFIQ akatumia fursa hiyo kuwataka wanawake wa kiislam hususani kinamama kuhakikisha wanawalea watoto wao katika maadili yaliyo mema ikiwemo kuwasomesha elimu ya dini pamoja na kuhakikisha mabinti wa kiislam wanavaa mavazi yenye stara.

Naye Sheikh wa mkoa wa Dodoma Alhaj MUSTAFA RAJABU akawataka wanawake wakiislam kuhakikisha wanawaongoza mabinti wao katika kutenda matendo mema na kufata tabia nzuri za uislam na kuachana na tabia ambazo sio za kiislam.

Pia Sheikh MUSTAFA RAJABU akatumia fursa hiyo ya kongamano liloandaliwa na Taasisi ya JAI Dodoma kuishukuru Taasisi hiyo ya JAI kutokana na misaada mbalimbali inayotoa katika jamii ikiwemo kuwahudumia wagonjwa na utoaji wa damu kwa watu wenye uhitaji.

Amir wa Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam JAI Dodoma Sheikh ALLY KANDA akitoa salam za Taasisi hiyo ya JAI Dodoma amesema kazi za Taasisi hiyo ni kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji katika jamii huku Mweka Hazina Msadizi wa Taasisi hiyo ya JAI Dodoma Ukhut ASIA MUHAMMED akisoma Risala kwa mgeni rasmi ameeleza malengo ya kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ikiwemo kuchangia damu kwa watu wenye uhitaji na kuwahudumia wagonjwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment