RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Mwalimu Nyerere Mhe.Stephen Wasira alipowasili katika viwanja vya Chuo Kampesi ya Karume Zanzibar, kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la Nne la Kumbukizi ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume, na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwanafunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Zanzibar Muzdalifa Ali Yassin aliyebuni Satalati Dish Control kwa ajili ya kusetia program za TV, wakati alipotembelea maonesho ya Wanafunzi Wabinifu wa Chuo hicho, kabla ya kufungua Kongamano la Nne la Kumbukizi ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume. na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Malimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana na Mkuu wa Chuo Prof.Shadrack Mwakalila.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkufunzi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Bububu Zanzibar Bw,Muhammad Kassim Muhammad akitowa maelezo ya kifaa cha “ IOT Based Hydro-ponics Monitoring System “ wakati akitembelea maonesho ya Wanafunzi Wabunifu wa vifaa mbalimbali katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Karume Bububu Zanzibar, kabla ya kulifungua Kongamano la Nne la Kumbukizi ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh.Abeid Amani Karume.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment