Thursday, March 24, 2022

ZAO LA ALIZETI SINGIDA LAPAMBA MOTO // RC MAHENGE ATAKA WAKULIMA WANUFAIKE

Mkuu wa Mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge Akiwa ameshika Alizeti Mbichi wakati alipotembelea mashamba  ya wakulima wa kubwa wa zao hilo Halmashauri ya Wilaya ya Singida hapo jana.

Mazao ya Alizeti yakiwa yamestawi na kunawili kwenye shamba  la wakulima wakubwa wa Halmashauri ya wilaya ya Singida.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge [Kushoto]  Akionyesha mfano wa mbegu  bora ya alizeti iliyopandwa na wakulima , akiwa ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Paskasi Muragili [kulia].

Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Nathalia Moshi Akisoma taarifa ya hali uzalishaji wa zao la Alizeti kwenye Halmashauri hiyo baada ya zaira ya mkuu wa mkoa wa Singida Kutembelea Mashamba ya wakulima. 


Alizeti ikiwa shambani 


Na Hamis Hussein - Singida

MKOA  wa  Singida  unatarajia kuzalisha  tani 581.9 za zao la alizeti  ambazo zitakwenda kuchangia kwa  kiwango kikubwa ongezeko la upatikanaji wa  mafuta ya kula nchini  ambalo hitaji lake halisi ni  takribani tani laki sita na  nusu.

Jitihada hizo pamoja na mambo mengine zinakwenda kupunguza gharama kubwa ya takribani Bilioni 500 ambazo serikali hulazimika kila mwaka kutumia kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.  

Kwa mujibu wa Takwimu za Mkoa mpaka sasa tayari ekari 239,700 za alizeti zimelimwa na kupandwa aina tofauti za mbegu za zao hilo zipatazo tani 469.

Hata hivyo akiwa kwenye ziara ya kutembelea mashamba mbalimbali ya alizeti yaliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida  Mkoani hapa jana , Mkuu wa mkoa Dkt. Binilith Mahenge aliagiza kuitishwa kwa kikao cha Wadau wa mnyororo wa zao hilo ili kwa pamoja kujadili namna nzuri ya kuhakikisha kunakuwa na bei nzuri ambayo itawanufaisha wakulima wote wa zao la alizeti.

“Tunategemea kuvuna mara mbili zaidi ya mwaka jana mavuno yatakuwa  makubwa kwahiyo chakukubaliana hapa tuandae kikao cha wadau waliotoa mbegu, wale waliolima na wenye viwanda ili tuangalie nani atachukua tani ngapi na kwa bei  ipi, isitokee wananchi wakaanza  kuangaika mtu akawa anachukua Mazao kwa bei ya chini” Alisema Dkt. Mahenge.

Dkt. Mahenge alisema kupitia vikao vya mkoa kuhusu mkakati wa kilimo cha alizeti  zilianishwa ekari zitakazozalishwa kwa mkoa wa Singida na ukafanyika mgawanyo kwa kila halmashauri ambapo serikali ilitoa ruzuku ya mbegu kwa wakulima jambo ambalo  limeongeza uzalishaji  akitolea mfano Halmashauri ya Wilaya ya Singida.

Mkuu wa mkoa wa Singida Akipewa Maelezo ya mashamba ya alizeti kwenye ziara hiyo.



Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge  akikagua kama kuna wadudu wanaweza kushambulia Alizeti iliyopandwa na wakulima. 


Matembezi ya kukagua mashamba ya wakulima wakubwa wa alizeti yakiendelea.

Akiwa Kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa  Mkuu wa wilaya ya Singida Mhandisi Pasikasi Muragili alisema  ikiwa mwenendo wa kilimo cha zao hilo utaendelea vizuri mkoa huo utachangia kiwango kikubwa kwenye uzalishaji wa mafuta hapa nchini kupitia mazao ambayo yamelimwa na wakulima.

Mhandisi Muragili alisema pamoja na kutofikia malengo ya  serikali ya kupata mbegu   walizoomba lakini wakulima walitafuta mbegu kutoka kwa wadau wengine hivyo kwa kiwango cha mbegu walizopanda wakulima hao kupata mavuno mengi  na kuisaidia kuongeza uzalisha mafuta yakutosha.  

Akiwasilisha taarifa ya uzalishaji wa Alizeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Afisa Kilimo Bi Nathalia Moshi  amesema katika msimu wa kilimo 2021/22 ilitarajia  hecta 38,936 na kuvuta tani 73,936 ambapo halmashauri hiyo  iliomba mbegu tani  195  kutoka  kwa wakala wa mbegu Asa lakini mpaka sasa wamepata mbegu tani 76.01  ambazo zimesambazwa katika kata 21 .

Nathalia aliongeza kuwa Halmashauri imeshirikiana na wadau mbalimbali wakiweo Mradi wa kukabiliana na Madhara ya Ukivo 19 unaofadhiliwa na mfuko wa kimataifa wa  maendeleo ya kilimo IFAD  ,Mwenge Sunflower , pyxus ,  Mount Meru Millers limited  kuwapatia wakulima mbegu za alizeti.

Mbegu Bora ya Alizeti ikiwa yamestawi Shambani



No comments:

Post a Comment