Saturday, March 5, 2022

ZAIDI YA WANAWAKE 500 WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO KATIKA KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

 


Naibu waziri wa maliasili na utalii Mhe.Mary Masanja (aliyeshika maiki) akizungumza na wanawake zaidi ya 500 ikiwa ni maandalizi ya safari yao ya utalii wa ndani kuelekea mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.



Zaidi ya wanawake 500 wakiwa katika maandalizi ya kuelekea mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni moja ya utalii wa ndani katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanamke duniani.

Na Agness Nyamaru,Arusha.

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani naibu waziri wa maliasili na utalii Mary Masanja amewataka wanawake wote kukumbuka kuwa wao ni moja ya nyenzo katika kujenga taifa hili la Tanzania.

Ameyasema hayo wakati wakijiandaa kuanza safari kuelekea ngorongoro katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,Masanja alisema tukio hilo Ni kuunga mkono juhudi za serikali za awamu ya sita zilizoanzishwa na rais Samia Suluhu Hassan ambapo wamechagua wiki hii ya wanawake duniani kulionyesha  bara la afrika,kuwa siku hiyo ni ya muhimu ikiwa wameongozana na zaidi ya wanawake 500 kwa ajili ya kwenda kutembelea mamlaka ya hifadhi hiyo ya ngorongoro ikiwa pia ni sehemu ya kuhamasisha utalii wa ndani.

“Tnapoenda kuona vivutio vyetu vya Tanzania sio kwa kutazama tuu lakini pia kwa kujifunza kwani kuna mambo mengi ya kujifunza vikiwemo viumbe hai pamoja na fuvu la mwanadamu wa kwanza ambalo huwezi kulikuta sehemu yoyote duniani,”alisema Waziri Masanja.

Aidha aliongeza kuwa  wanaamini Ngorongoro ni bustani ya Eden hivyo wameona katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hawawezi kukosa kwenda, ikiwa suala la kukuza utalii wa ndani linaanza na mtu mmoja mmoja lakini pia  ni sehemu ya kutekeleza na kuunga mkono juhudi za Mh.Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye amekuwa mshiriki namba moja wa kutangaza utalii wa nchi hii.

"Nifuraha kubwa kuona kundi hili la kinamama waliojitokeza kuunga mkono suala zima la kukuza utalii wa ndani na wanawake wanaweza kuukuza utalii wa ndani ikiwa wanaonyesha kwa vitendo kwa kulipa fedha zao kutembelea hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari zao wenyewe kama wazalendo,"alisema Masanja.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa Tanzania imefunguka, ikiwa sambamba na utalii kuwa vizuri kwa sasa tofauti na kipindi cha nyuma Kutokana na janga la korona lililoikumba dunia, hivyo kwa sasa kupitia hilo wanaendelea kuitangaza nchi kwa watalii wanaoingia ikiwa wao kama wazalendo wataungana kwa ajili ya kwenda ngorongoro kwani ni mojawapo ya utalii wa ndani.

Alisema kuwa serikali ipo pamoja nao ikiwa ni siku ya pili ya juma la maadhimisho ya siku ya wanawake duniani inayokwenda sambamba na tukio hilo la uhamasishaji wa utalii wa ndani ambapo wao kama wazalendo wanaunga mkono juhudi za mh rais alizozianzisha Kutokana na loyal tour.

Kwa upande wake balozi wa utalii wa jumuiya ya Afrika Mashariki Sharon Ringo alisema kuwa anayofuraha kubwa sana ya kuwa sehemu ya kuutangaza utalii  wa ndani kwenda kujionea kivutio vya Tanzania ikiwa ni mojawapo ya bustani  ambayo Mungu aitukia Tanzania.

Hata hivyo balozi huyo alisema kwamba sio wanaume pekee yao wanaweza kufanyakazi hata wanawake wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla ili kuleta maendeleo katika jamii.

No comments:

Post a Comment