Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua birika la kunyweshea mifugo wakati akizindua mradi wa uhifadhi na utunzaji chanzo cha maji cha chemchem za Qang'dend na mito ya Baray na Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha juzi.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Dk.George Lugomela, akitoa taarifa ya mradi huo.Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Wanyenda Philip Kutta, akitoa taarifa fupi wakati wa uzinduzi huo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Musa Matoroka akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Cecilia Paleso, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba, akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Karatu, John Lucian, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia Maji Bonde Dogo la Eyasi (JUWAMABOE) Maiko Silaa akitoa taarifa kwenye uzinduzi huo.Aliyekuwa akikaimu nafasi ya Afisa Maji Bonde la Kati, Danford Samson (kushoto) akipongezwa baada ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso kumtangaza kuwa Afisa Maji Bonde la Kati.Aliyekuwa akikaimu nafasi ya Afisa Maji Bonde la Kati, Danford Samson na sasa ni Afisa Maji Bonde la Kati, akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo.
Mhandisi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati Moses Sulumbi, akiwajibika kwa kurekebisha koki ya kufungulia maji katika bomba lililopo eneo la mradi huo.
Muonekano wa tenki la maji lililopo kwenye eneo wa mradi huo.
Maofisa wa Bodi ya Maji Bonde la Kati wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi huo. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi, Nelea, Bundala, Hapiness Mlingi na Neema Wilson.
Wasanii wa Kikundi cha Sulgadatoga kutoka Kijiji cha Makeckchand wakitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (katikati) akiserebuka na Wasanii wa Kikundi cha Sulgadatoga kutoka Kijiji cha Makeckchand wakati walipokuwa wakimpokea.
Uzinduzi ukiendelea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Mhandisi Samson Babala (kushoto) na Afisa wa Bonde hilo, Asante Swai wakiwa kwenye uzinduzi huo.Mtaalam wa masuala ya maji wa Bonde la Kati, Salim Lyimo akiwa kwenye uzinduzi huo.Mhandisi wa Mazingira Nyacheri Mramba akiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ya uzinduzi ikiendelea. |
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Na Hamis Hussein - Karatu ARUSHA
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amezindua mradi wa uhifadhi na utunzaji chanzo cha maji cha chemchem za Qang'dend na mito ya Baray na Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha.
Akizindua mradi huo Aweso, alisema Serikali kupitia wizara hiyo itatenga kiasi cha Sh.4 Bilioni katika bajeti ijayo inayoanza mwaka huu kwa ajili ya kutatua changamoto ya maji inayolikabili jimbo la Karatu.
Aweso aliyasema hayo juzi Tarehe 1 Machi 2022 wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa Kijiji cha Qang'dend kilichopo kata ya Mang'ola Tarafa ya Eyasi wilayani Karatu baada ya kuzindua mradi huo.
Alisema mji wa Karatu ambao ni wa maendeleo, kiuchumi na wa kiutalii unakabiliwa na changamoto ya maji hivyo unahitajika kusaidiwa kupata maji na hasa ukizingatia kuwa hauna umaskini wa vyanzo vya maji kama yalivyo maeneo mengine.
"Nimepata taarifa mahitaji ya maji mji wa Karatu ni lita milioni 5 lakini uzalishaji wa maji kwa sasa ni lita milioni 1.6, Karatu inahitaji kusaidiwa,nataka nikuhakikishie mbunge tunakwenda bungeni katika bunge la bajeti jimbo la kwanza kuliangalia itakuwa ni Karatu na katika bajeti tutatenga Sh.4 Bilioni kutatua tatizo la maji," alisema Waziri Aweso.
Alisema kumekuwa na changamoto katika suala la fedha zinazotolewa na serikali hivyo wataalamu wa Karatu wafahamu kuwa serikali haileti fedha hizo kwa ajili ya kuziweka mfukoni halafu matokeo hayaonekani,hapana.
"Tumewahi kusema na tunaendelea kusema vipo vya kuchezea ukishiba chezea kidevu au kitambi chako si fedha za miradi ya maji, tutakushughulikia na mimi bwana ni kijana ukinizingua tunazinguana, ..wabunge hizi ni fedha na wala hazina mjadala twendeni tukazisimamie ili wananchi wanufaike na upatikanaji wa maji," alisema.
Waziri Aweso aliwagiza viongozi wa mabonde yote ya maji nchini kuhashirikisha wanawashirikisha wananchi katika suala la kulinda na kutunza vyanzo vya maji vilivyopo.
"Jamii ukiishirikisha utafanikiwa, jamii usipoishirikisha utakwama,kwa hiyo watu wetu wa raslimali za maji niwaombe suala la kulinda na kutunza vyanzo vya maji pamoja na bonde wananchi wanahitaji kushirikishwa," alisema Waziri Aweso.
Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya viongozi na hata wananchi wanajua umuhimu wa kujengewa mradi tu lakini wanasahau suala la kulinda na kutunza vyanzo vya maji.
"Hatuwezi kuona leo shughuli za binadamu zinafanyika katika vyanzo vya maji, hatuwezi kuona uchimbaji madini unafanyika katika vyanzo vya maji mtu wa bonde leo upo tu ofisini umekaa huwezi kuona,lazima ushirikishe jamii na viongozi wa eneo husika," alisema.
Aweso alisema haipendezi na wala haifurahishi kuangalia katika luninga (TV) mwananchi ameshalima mazao yake kwenye chanzo cha maji halafu afisa wa bonde anakwenda na panga kuyakata kwani wakati mwananchi analima huyo afisa alikuwa wapi.
"Hivi karibuni na ninyi ni mashahidi hali iliyoikumba jiji la Dar es Salaam kwenye vyanzo vya maji vya Ruvu chini na juu vilikauka kabisa jiji la Dar es Salaam likawa halina maji kabisa mimi Waziri wa Maji nikaona kwa hapa ilipofikia natakiwa niitwe waziri wa ukame," alisema.
Aweso alisema wananchi lazima watambue kuwa suala la mazingira lina kisasi ambapo ukiyaharibu mazingira na wewe yatakuharibu na ukiyatunza na wewe yatakutunza hivyo hakuna asiyejua maji chanzo kikibaribika kitapotea na mateso yake ni makubwa.
Alisema miaka ya nyuma maeneo mengi yalikuwa na chemchem za maji lakini leo hii hazipo zimekauka kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya wananchi kwa kulima katika vyanzo vya maji na kuendesha shughuli za ufugaji.
"Niwaombe sana ndugu zangu maji ni uhai, maji hayana mdabala, maji si kama wali ambao ukikosa wali unaweza ukala ugali,ukikosa ugali unaweza ukala ndizi, mtu anauyekosa maji maana yake anakaribisha maradhi," aliongeza waziri Aweso
Kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Bodi ya Maji Bonde la Kati ya kutekeleza mradi huo, Waziri wa Maji, Aweso alitangaza kumpandisha cheo aliyekuwa akikaimu nafasi ya Afisa Maji Bonde la Kati, Danford Samson kuwa Afisa Maji Bonde la Kati.
"Huyu Kaimu Afisa Bonde ya Maji Bonde la Kati 'Danford Samson' ukimwangalia mpole unaweza ukawa na mashaka juu ya utendaji wake wa kazi, kwa heshima na taadhima naomba leo nimteue awe Afisa Maji Bonde la Kati kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya akishirikiana na wafanyakazi wenzake," alisema.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Dk.George Lugomela, alisema hapa nchini kuna jumla ya vyanzo vya maji 1,867ambavyo vinatoa huduma lakini vipo katika hatari ya kuharibiwa.
Dk.Lugomela alisema vyanzo vya maji ambavyo vimewekewa mipaka ni 180,vilivyotangazwa katika gazeti la serikali na kupata GN ni 18 na vyanzo 45 vipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali vinasubiri kwa ajili ya kutangazwa.
"Tunataka ifikapo mwaka 2025 vyanzo vyote vitakuwa vimewekewa mpaka na kuvitunza ili viweze kutoa huduma endelevu na tunamshukru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo," alisema Dk. Lugomela
Mradi wa chanzo cha maji cha chemchem Qang'dend unategewa na wananchi 44,091 wa vijiji saba vya tarafa ya Eyasi.
No comments:
Post a Comment