Wednesday, March 16, 2022

WAZIRI MULAMULA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI WA MALAWI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiongea na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
 
Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula mara baada ya kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho
 
 
Mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda
 
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda katika picha ya pamoja na maafisa walioambatana nao.

Na Waandishi wetu, Dar
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi nchini Mhe. Andrew Kumwenda leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
Baada ya kupokea nakala ya hati hizo Balozi Mulamula amemuahidi Balozi mteule ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi wakati wote atakaokuwepo nchini.
 
“Leo nimepokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Malawi na tumefarijika kwa Mhe. Rais Chakwera kumteua Balozi huyu mara baada ya Balozi wa awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, hii ni ishara ya uhusiano wa karibu, undugu na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Malawi,” amesema Balozi Mulamula
 
Kwa upande wake Balozi Mteule wa Malawi Mhe. Andrew Kumwenda amesema kuwa Malawi na Tanzania siku zote zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na jukumu langu hapa kama Balozi ni kuhakikisha uhusiano huu unazidi kuku ana kuimarika.
 
“Tanzania inatekeleza Diplomasia ya Uchumi na vivyo hivyo Malawi………kwa hiyo sisi wote tuna lengo moja, na nitahakikisha Tanzania na Malawi zinashirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” Amesema Balozi Kumwenda.

No comments:

Post a Comment