Sunday, March 20, 2022

JAI TOENI ELIMU YA LISHE KWA JAMII ILI KUONDOA TATIZO LA UTAPIYAMLO DODOMA_MHE. SHEKIMWERI






Mkuu wa wilaya ya dodoma mjini JABIR SHEKIMWERI ameitaka Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) ambayo inajishuhulisha na utoaji wa msaada wa huduma katika jamii kuweka mkakati na mpango wa utoaji elimu ya lishe kwa jamii hususani kwa kinamama wajawazito ili kuondoa tatizo la lishe kwa watoto katika jiji hilo.

JABIR SHEKIMWERI ametoa rai hiyo katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma alipowatembele wagonjwa kuwajulia hali na kuwapatia huduma ya uji iliyoandaliwa na Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa wa Dodoma ambapo ameisisitiza JAI kujikita katika utoaji elimu ya lishe ili kusaidia kuondoa tatizo la utapiamlo kwa wakazi wa jiji hilo .

Aidha JABIR SHEKIMWERI amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ya (JAI) na kuahidi kuipatia taasisi hiyo eneo la uwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za taasisi hiyo haili itakayosaidia (JAI) kuendelea kutoa huduma katika jamii

Kwa upande wake Amiri wa Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa wa Dodoma ALLY KANDA akaeleza huduma zinazotolewa na taasi hiyo katika jamii  ikiwemo kuwalisha wagonjwa,kuwasaidia huduma za dawa na kusafirisha kwenda makwao.

Naye Mratibu wa Taasisi hiyo ya Taasisi ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) mkoa wa Dodoma MOHAMEEDI OTHUMANI akatumia fursa hiyo kueleza changamoto zinazoikabili taasisi hiyo ikiwemo ukosefu wa ofisi huku akiiomba serikali kuiwezesha Taasisi hiyo kuweza kupata ofisi.

No comments:

Post a Comment