Thursday, February 3, 2022

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA DSTV KWA KUTANGAZA MAUDHUI YA KITANZANIA

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa  ametoa Kongole kwa Kampuni ya Multichoice Tanzania (DSTV) kwa kurusha maudhui ya kitanzania hususan Muziki na Filamu ambayo yameleta manufaa kwa wasanii.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Februari 3, 2022  wakati alipokutana na  kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Jacqueline Woiso katika ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma.

“Nitakutana na wasanii wote wakiwemo waigizaji na wanamuziki na kufanya nao mazungumzo, hii itatuwezesha kujua changamoto zao na mahitaji yao katika kufanya kazi zao za sanaa na hili ningeomba ushirikiano kutoka kwenu Multichoice Tanzania ili kuweza kufanikisha,”amesema Mhe. Mchengerwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo, ameahidi ushirikiano wa karibu na Wizara katika kuhakikisha sanaa inakuwa na wasanii wanapata kipato kutokana na kazi zao.

No comments:

Post a Comment