Wednesday, February 23, 2022

WAKULIMA NZEGA WAPO TAYARI KWA UJENZI NA UKARABATI WA MRADI WA UMWAGILIAJI IDUDUMO

Kulia, Mhandisi Mwinchuma Tengeneza akimkabidhi kablasha la eneo la kazi ya Ujenzi na Ukarabati wa miundombinu, katika skimu ya kilimo cha
Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main
Constructors Ltd Bw. Basil Clement (kushoto).

Picha Ikionesha eneo la Utoro wa Maji katika Bwawa la Idudumo ambalo litavunjwa na kujengwa upya.

Wapili kutoka kulia, Meneja Mradi wa Ujenzi na Ukarabati wa Skimu ya
Umwagiliaji Idudumo Bw. Juma Kibori akiwaonesha wawakilishi wa viongozi wa Halmashauri ya Nzega mji na wataalam ramani ya ujenzi na ukarabati wa eneo la mradi

Picha ikionesha sehemu ya eneo la Bwawa Idudumo, ambalo litafanyiwa ukarabati katika awamu nyingine ya mradi.

Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati w mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kw asilimia mia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa  zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu katika skimu hiyoutasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua,tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na  kuweza kuleta madhara kwa mazao.

“Naamini kuwa baada yau jenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi .”Alise Mkulima huyo”Alisema

Akizungumza wakati wa makabithiano hayo,Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema eneo la skimu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga chenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo,lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.

Aliendelea kusema kuwa,awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane,utaboresha miundombinu nakusaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.

No comments:

Post a Comment