Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na washiriki wa Mkutano wa umoja Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi za jumuiya ya afrika mashariki
Mkutano wa Umoja wa Tamisemi ukiendelea jijini Arusha.
Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya Pamoja na washiriki wa wa umoja Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi za jumuiya ya afrika mashariki.
Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa akikata keki wakati akifunga mkutano wa umoja wa Tamisemi Afrika Mashariki.
Mhe. Innocent Bashungwa akipeana mkono na moja ya viongozi walioashiriki Mkutano wa Umoja wa Tamisemi Afrika Mashariki siku ya jana February 9 2022.
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.
Innocent Bashungwa amesema Tanzania inajivunia mafanikio makubwa tangu ichukuwe
nafasi ya Uenyekiti kwenye Umoja wa Wizara zinazohusika na Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Waziri
Bashungwa amesema hayo jijini Arusha wakati akihitimisha Mkutano wa Umoja wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wa Nchi za Jumiya ya Afrika Mashariki
uliofanyika Februari 7 hadi 9, 2021.
"Katika kipindi hiki tunajivunia
umoja huu kwa kuingia hatua ya kusaini makubaliano na Sekretarieti ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki ili kuboresha ushirikiano wa wizara zinazohusika na Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa ndani ya Jumuiya yetu,"
amesema Mhe. Bashungwa.
Waziri
Bashungwa ameeleza kuwa, katika mkutano huo yamejadiliwa mambo mbalimbali
ikiwemo kujitayarisha kwa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kufufua uchumi baada
ya UVIKO-19 na mitazamo ya jukumu la Serikali za Mitaa, vipaumbele na hatua za
kimkakati za EAC.
Waziri
Bashungwa amesema kuwa, katika kipindi ambacho Tanzania ni mwenyekiti wa umoja
huu itaendelea kukuza mazungumzo kati ya mawaziri na Serikali za mitaa ili
kushughulikia changamoto zinazokabili katika ngazi ya mtaa.
Vilevile,
amesema Tanzania itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika kurasimisha sekta ya Serikali za Mitaa ndani ya jumuiya hiyo
na kuendelea kutoa nafasi ya kubadilishana ujuzi, taarifa, mbinu bora na
ubunifu kwa ajili ya utawala wa ndani.
Tanzania
ni nchi Mwenyekiti wa Umoja wa Wizara zinazohusika na Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tangu Oktoba 2021
ambapo Umoja huo unaongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe.
Innocent Bashungwa.
No comments:
Post a Comment