Friday, February 11, 2022

MACHINGA IRINGA WANAMGOGORO NA MEYA NA SIO KIONGOZI MWINGINE

 katibu wa MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph akiongea na wafanyabiashara wagodo wadogo manispaa ya Iringa wakijdali mstakabali wao wa kuhama maeneo ya mashine tatu na miomboni

katibu wa MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph akiongea na wafanyabiashara wagodo wadogo manispaa ya Iringa wakijdali mstakabali wao wa kuhama maeneo ya mashine tatu na miomboni

Na Fredy Mgunda,Iringa

Uongozi wa umoja wa wafanyabisahara wadogo wadogo (MACHINGA) Manispaa ya Iringa wamesema kuwa anaekwamisha zoezi la wao kupangwa vizuri ni meya wa manispaa ya Iringa na sio kiongozi mwingine na kusababisha mgomo wa kwenda eneo la welfare kufanyia shughuli zao za kibiashara. 

Akizungunza na blog hii katibu wa MACHINGA mkoa wa Iringa Joseph Kilienyi alisema kuwa wamekuwa wakifanya majadiliano mara kwa mara na viongozi mbalimbali wa wilaya na mkoa wa Iringa juu ya swala la MACHINGA kuhamia katika eneo la Makabuli ya Mlandege lakini kikwazo kimekuwa kwa meya wa manispaa ya Iringa.

Alisema kuwa wamewapangia eneo ambalo sio rafiki kwa biashara ambazo wanazifanya hivyo wameamua kugoma kuondoka katika maeneo ambayo wanafanyia biashara hivi sasa.

Kilienyi alisema kuwa serikali ya manispaa ya Iringa imewapangia wahamie katika eneo la welfare ambalo wanadai ni dogo halafu sio Rafiki kwa baishara ambazo wanafanya kwa kuwa ni vigumu wateje kuwafikia katika eneo hilo.

Alisema kuwa hayo yote yanakuja kwa shirinikizo la Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada ambapo wahajui anamaslai gani na maeneo hayo yote mawili ambayo anataka machinga waende kufanyia biashara zao.

Kilienyi alisema kuwa waliushauri uongozi wa wilaya,mkoa na manispaa ya Iringa kuwa eneo ambalo ni Rafiki kwa ajili ya biashara za MCHINGA ni pembezoni mwa makaburi ya Mlandege ambako kuna mzunguko mkubwa wa wananchi na kwao itakuwa rahisi kufanya biashara zao.

Aliongeza kuwa mara baada ya kuona swala hilo limekuwa gumu kwao walipeleka hoja binafsi kwenye baraza la madiwani ili madiwani waweze kuijadili kwa kina swala hilo lakini Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada aliitupilia mbali hoja jambo ambalo wanadai lilizua maswali mengi vikwani mwao. 

Kilienyi alisema kuwa uongozi wa manispaa ya Iringa ulishauriwa kuweka uzio kuyazunguka makaburi hayo na sehemu ya nje ya uzio ndio yatakuwa Rafiki kwao kufanyia biashara tofauti na maeneo ambayo wanapangiwa bila kushirikishwa na kiongozi huyo. 

Kwa upande wake mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa alisema kuwa haoni hoja ambayo imekuwa ikimpelekea meya Ngwada kulikataa ombi la wafanyabiashara hao kwenye kufanyia biashara zao pembezono mwa makaburi ya Mlandege. 

Mpelembwa alisema kuwa uongozi wa mkoa Iringa chini ya mkuu wa mkoa wa Queen Sendiga na mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Moyo ulikubari ombi lao lakini meya amekuwa kikwazo kwa kulikataa ombi hilo. 

Naye aliyekuwa mwenyekiti wa MACHINGA mkoa wa Iringa Zeche Zabron alisema kuwa wafanyabisha hao wanatakiwa kwenda katika makaburi ya Mlandege tu na sio sehemu nyingine kwa kuwa makaburi hayo yanaweza kuondolewa kwa kuwa yamekaa miaka mingi ambayo kisheria yanatakiwa kuondolewa kwa kufuatatu utaratibu husika.

Alisema hakuna sheria inayokatakaza makaburi kuhamishwa hivyo ameutaka uongozi wa manispaa ya Iringa kuhakikisha wanayaoondoa makaburi hayo kwa mujibu wa sheria za nchi kama ambavyo inatakiwa la sio watalazimika kwenye mahakani kwa hoja ya kuyaondoa makaburi hayo.

Zeche alisema kuwa tatizo pale kuna kaburi la babu yake meya wa Iringa Ibrahim Ngwada ndio maana imekuwa tatizo kwake lakini makaburi yale tayari yameshapitwa na muda hivyo yanatakiwa kuondolewa au kuwekea uzio ili MACHINGA wahamie kufanya biashara zao pale.

Alisema kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo (MACHINGA) mkoani Iringa wataendelea kuugomea uongozi wa manispaa ya Iringa kuhama katika eneo la mashine tatu na miomboni ambalo wanafanyia biashara zao hivi sasa hadi pale watakapo ambiwa wahamie Mlandege.

Akijibia kero hizo Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa kila hatua wanayoifanya ya kuwahamisha MACHINGA katika manispaa hiyo wamekuwa wakiwashirikisha viongozi wao mara kwa mara anashangaa kuona wameanza kuyageuka majadiliano yao.

Alisema kuwa walikubaliana na viongo wa umoja huo kuwa eneo Rafiki kwa biashara yao ni eneo la welfare na serikali ikawekeza fedha nyingi ambazo zimetumika kujenga mabanda ya kufanyia biashara na yamekamika sasa anashangaa kuona kumeanza maneno mengine ambayo hayana afya kwa maendeleo ya manispaa ya Iringa.

Ngwada alisema kuwa viongozi wa MACHINGA wamekuwa wakilitaka eneo la makaburi ya Mlandenge jambo ambalo ni gumu kufanyika kutokana na historia ya makaburi hayo.

Ngwada alisema kuwa ili kuyaondoa makaburi hayo ni lazima kuwashirkisha wananchi,viongozi wa dini wizara husika na kutathimini gharama halisi ya makaburi hayo na kuingalia sheria inasema na vyote hivyo havijafanyika na viongozi wa MACHINGA Iringa wanataka tu yaondoke wapewe eneo hilo wafanyie biashara.

Alisema kuwa kuhusu hoja yao kupeleka kwenye baraza la madiwani haikufuata wala haikuzingatia sheria na kanuni za baraza la madiwani wa manispaa ya Iringa ndio maana hoja hiyo haikusomwa mbele ya madiwani na wananchi wengine waliohudhuria baraza hilo.

Alisema kuwa watu waliozikwa katika eneo hilo wanathimini kwa mchango wa kimaendeleo walioufanya hadi kuifikisha manispaa ya Iringa ilipofika hivyo sio japo jepesi kiasi hicho cha kuyaondoa makabuli hayo.

Ngwada alisema kuwa kuna maeneo mengi ambayo MACHINGA wa Manispaa ya Iringa wanatakiwa kufanyia biashara sio eneo ambalo holo wanalolihitaji kwa kutumia mashinikizo bila kujali wataalam wanasema nini

No comments:

Post a Comment