Wednesday, February 16, 2022

MACHINGA IRINGA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUANZISHA SACCOS YA MACHINGA

Mwenyekiti wa machinga mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa akiongea na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa SACCOS ya machinga mkoani Dar es Salaam ambapo waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi
Mwenyekiti wa machinga mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa akiongea na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa SACCOS ya machinga mkoani Dar es Salaam ambapo waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa mgeni rasmi 

 Na Fredy Mgunda,Iringa. 

WAFANYABIASHARA wadogo wadogo (MACHINGA) mkoa wa Iringa wamesema kuwa kupatikana kwa SACCOS ya umoja huo nchi nzima kupatikana kwa mitaji na kukuza mitaji kwa kuwa wanaukakika watakopa kwa riba nafuu.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa machinga mkoa wa Iringa Yahaya Mpelembwa alisema kuwa MACHINGA Tanzania wanaenda kuzindua SACCOS ya wafanyabiashara hao siku ya tarehe 19/02/2022 mkoani Dar es salaam na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mpelembwa alisema kuwa wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kwa kuamua kuanzisha SACCOS ya machinga nchi nzima kwa kuwa itasaidia kukuza mitaji ya wafanyabiasha hao.

Alisema kuwa amekuwa Rais wa kwanza kuweka historia ya kukutana kundi hilo la wafanyabiashara wadogo wadogo na kutambua mchango wao katika kukuza uchumi wan chi.

Mpelembwa alisema kuwa wafanyabiashara hao wamekuwa wanakilio cha muda mrefu cha kutokopesheka kwa kuwa walikuwa hawana dhamana hivyo kitendo cha serikali kuanzisha SACCOS hiyo itakuwa mchombozi kwao.

Alisema kuwa kuzinduliwa kwa SACCOS hiyo kutakuwa na faida ya wafanyabishara hao kuanza kukopa kwa riba nafuu tofauti ilivyo hivi sasa ambavyo wanahangaika kupata mitaji ya kukuza biashara zao.

Mpelembwa alisema kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo (MACHINGA) mkoa wa Iringa wanaungana na wafanyabiashara hao nchi nzima kukifanya chombo hicho kuwa imara zaidi kwa kuwasaidia mitaji machinga wote.

Alisema kuwa swala la mitaji kwa machinga mkoa wa Iringa kimekuwa kikwazo kikubwa katika kukuza biashara wanazozifanya hivyo kuwepo kwa chombo hicho kutasaidia kukuza mitaji yao.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo (MACHINGA) mkoa wa Iringa walisema kuwa kuundwa kwa chombo hicho kutasaidia kukuza biashara zao na kuwapelekea kuwa wafanyabiashara wakubwa.

Walisema kuwa wanampongeza na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suhulu Hassan kwa kulikumbuka kundi la machinga ambalo kwa miaka mingi lilikuwa limesaulika na viongozi wengine. 

Waliongeza kuwa kuzinduliwa kwa chombo hicho kutasaidia kukuza uchumi wa wafanyabiashara hao na wananchi wote kwa ujumla kwa kusaidia kukuza maendeleo ya nchi na kuongeza pato la wananchi.

No comments:

Post a Comment