Saturday, February 12, 2022

Hakuna mradi wa barabara za vijijini utakaokwama’ WAZIRI MKUU









OR-TAMISEMI

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasism Majaliwa Majaliwa amesema hakuna barabara ya vijijini wala mjini itakayokwama kujengwa kwa kukosa Fedha kwa sababu Serikali imeelekeza  fedha nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa barabara za  ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mhe. Majaliwa ameyasema hayo  wakati wa kufungua kikao kazi kati ya TAMISIMI, TARURA na wakandarasi kilichofanyika jijini Dodoma.

Alisema Serikali imefanya juhudi katika kuijengea uwezo TARURA ili iweze kutekeleza makujumu yake na kuiongezea fedha kutoka Sh bilioni 247.5 ilipoanzishwa mwaka 2017 hadi kufikia Sh bilioni 719.61. 

“Fedha hizi zinajumuisha shilingi bilioni 127.50 kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali, shilingi bilioni 243 kutoka Mfuko wa Barabara, shilingi bilioni 322.15 kutoka katika tozo ya shilingi 100 kwa lita ya mafuta ya petroli na dizeli na shilingi bilioni 30.44 kutoka kwenye ushuru wa maegesho wa magari na hizi zote  ni kutoka katika Fedha za ndani tu sawa ambayo ni ongezeko la asilimia 204.3.

Mhe. Majaliwa alisema kwa sasa takribani Sh trilioni 1 zimeelekezwa kwenye barabara za mijini na vijijini kutoka Serikali kuu, Tamisemi, mfuko wa barabara, tozo ya mafuta, maegesho ya magari na fedha zinazotolewa kwenye miradi inayotekelezwa na wadau wa maendeleo kama Dmdp, Rise, Tactic na Agri business.

“ Niwahakikishie wakandarasi wanaopewa kazi na Serikali kuwa hakuna changamoto ya fedha, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajitahidi kutafuta fedha hivyo mkipewa kazi mtalipwa kwa wakati, na hakuna barabara itakwama, ukisiani mkataba kazi lazima ianze.

“ Zile kauli za wakandarasi wanazosema ukitaka ufilisike fanyakazi na Serikali hazitakiwi kuwepo kwasababu fedha zipo na mtalipwa kwa wakati.

Aidha, Mhe. Majaliwa alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakandarasi wa ndani kuungana ili waweze kupewa kazi kubwa na kuwa hali ya sasa ya kila mkandarasa kufanya kivyake inawanyima fursa na kusisitiza kuwa haipendezi kazi kubwa zikatolewa kwa wakandarasai wa njje ambapo wa ndani wangeungana wangeweza kufanya kazi hiyo

No comments:

Post a Comment