Na Mathias Canal, Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amekabidhi Ofisi kwa Waziri mpya wa Kilimo
Hussein Bashe huku alieleza kuwa amekabidhi kwa mtu anayejua vizuri.
Hayo ameyasema jijini Dodoma
leo tarehe 11 Januari 2022 wakati akikabidhi Ofisi kwa Waziri huyo Mara baada
ya kuapishwa rasmi jana ambapo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru watumishi wa
wizara hiyo kwa ushirikiano waliompa na kuwaaga.
"Nakabidhi ofisi kwa mtu
anayejua wizara hii maana nilipokuja hapa nilimkuta mheshimiwa Hussein Bashe tumefanya
kazi pamoja anaifahamu vizuri ofisi na mengi yaliyomo humu anayafahamu,
nakutakia kila la heri kwenye utumishi wako,".amesema Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akikabidhi ofisi.
"Mimi na Bashe tumefanya
kazi pamoja kwa ushirikiano mkubwa Kuna wakati mambo yalikuwa yakiwaka moto
tunakutana haraka usiku ili kujadili na kutoka na msimamo mmoja," amesema
Profesa Mkenda
Amesema kilimo ni changamoto kubwa lakini kwa sasa kipo mikono salama na kuwataka waliobaki kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizobaki.
Ametumia nafasi hiyo
kuwashukuru watumishi wa wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa wakati wa
mchakamchaka wa utekelezaji majukumu yake.
Akizungumza Mara baada ya
kukabidhiwa ofisi, Waziri Bashe amesema katika kipindi cha mwaka mmoja
walichofanya kazi kwa pamoja misingi mizuri imejengwa ambayo yeye ataendelea
kuifanyia kazi ili kuhakikisha kilimo kinasonga mbele.
"Tumefanya kazi mwaka mmoja ambao tumejenga misingi mizuri ambayo tutaendelea nayo sababu najua juhudi tulizofanya kufikia sehemu nzuri, tuna changamoto nyingi zinatukabili hivyo lazima tuzifanyie kazi, kwa kipindi cha mwaka mmoja nimepata ujuzi mkubwa kutoka kwako hivyo nakuahidi hakuna kilimo bila teknolojia wala Sayansi hivyo nitaendelea kukusumbua" Amekaririwa Mhe Bashe
Kadhalika, Waziri Bashe
amemuimba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Adolf Mkenda kutenge fedha
kwa ajili ya kwenda kusomesha wataalamu wazuri wa kilimo nje ya nchi.
MWISHO
Namuamin Sana huyu prof
ReplyDeleteBashe ni jembe kifupi hizi wizara zimekutan na mafundi
ReplyDelete