Friday, January 28, 2022

TANZANIA, MAREKANI ZAKUBALIANA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania  wakipewa maelezo kutoka kwa Mark Davidson ( wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili katika  Bodi ya Utalii ya Dallas ambapo wamefanya ziara ya  kutembelea katika ofisi hizo kwa lengo la kujifunza namna Bodi hiyo inavyofanya kazi zake katika kutangaza  utalii poamoja na kuanzisha ushirikiano wa kufanya kazi kwa pamoja kati ya Bodi hiyo na Bodi ya Utalii  Tanzania 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA,Brigedia Jenerali ( Hamisi Semfuko)  akiwa na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani  n  Dkt. Elsie Kanza ( wa kwaza kulia)  wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendahji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo yao wamekubaliana  kuimarisha ushirkiano  katika uhifadhi wa wanyamapori
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania  wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mshauri wa Kimataifa  wa Uwindaji wa Kitalii,  Balozi Mhe. Jean Philips (wa tano kulia ) mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya uhifadhi wa wanyamapori na uendelezaji Utalii hususani Uwindaji wa Kitalii. Wa tano kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza na wa tano kulia ni Brigedia Jenereli, Hamisi Semfuko
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa nne kulia)   akiwa na  Balozi wa Tanzania nchini Marekani  n  Dkt. Elsie Kanza (katikati)  pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA,Brigedia Jenerali  Hamisi Semfuko ( wa nne kushoto)  wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Makumbusho ya aliyekuwa Rais wa Marekani, John Kennedy 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa tano kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wake alioambatana nao kutoka Tanzania  wakiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Utalii wa Dallas  Balozi Mhe. Mark Thompson (wa tano kushoto ) mara baada ya kikao kilichofanyika baina yao ambapo wamekubaliana kuanzisha ndege ya moja kwa moja kutoka Tanzania kwenye nchini Marekani katika Jimbo la Dallas. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza na wa nne  kulia ni Brigedia Jenereli, Hamisi Semfuko

Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani  zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji   pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii 

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro  (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya vikao vya ana kwa nyakati tofauti  kwa lengo la kujifunza namna wanavyoendesha shughuli za utalii pamoja kukuza ushirikiano baina ya pande zote mbili 

“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Jimbo la Dallas  pamoja na kuangalia namna tunavyoweza kuliteka soko la watalii katika Jimbo hilo, tumejadili mikakati ya kuanza na watalii ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu katika jimbo hilo lengo likiwa ni kupata soko la uhakika la  watalii wengi zaidi katika  siku za usoni ” Amesema Waziri Ndumbaro

Akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Jimbo la Dallas Liliana Rivera, Dkt. Ndumbaro amesema moja ya shabaha kubwa ni kuhakikisha kunaanzishwa  ndege ya moja kwa moja ya kutoka Tanzani kwenda Dallas ambapo amesema itaweza kusaidia  Watanzania ambao ni watalii kwenda Dallas na Watalii kutoka Dallas kutembelea Tanzania

” Tanzania imeshaanzxa mazungumzo na Uongozi wa Jimbo hilo ili kuhakikisha hilo linafanikiwa na hivi wiki lijalo Mkurugenzi wa Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) atakuja Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzio hayo

Katika ziara hiyo pia,   Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mchezo wa Gofu nchini Marekani, Bruce Davidson ambapo Dkt.Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuinadi Tanzania kuwa  ipo  tayari kuwa  Mwenyeji wa mashindano makubwa  ya mchezo wa gofu yatayohusishwa Wachezaji mahiri wa mchezo huo 
 
“ Mchezo wa gofu ni mchezo unaochezwa na watu wenye fedha nyingi hivyo kuwa wenyeji wa mashindano hayo tutapata fursa ya. kutangaza vivutio vya utalii kwa gharama nafuu kwa sababu wachezaji wakubwa pamoja na watu mashuhuri watakuja Tanzania , kupitia umaarufu wao vyombo vikubwa vya habari duniani vitaambatana nao kwa ajili ya kuripoti yatakayojiri” ameongeza Waziri Ndumbaro

Aidha, Katika mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro wamekubaliana kutangaza vivutio vya utalii kupitia mchezo huo kwa kutumia vyombo vya habari vya kimataifa vitakavyotumiwa katika kutangaza mchezom huo

Katika hatua nyingine, Waziri Ndumbaro  amekutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo hayo wamezungumza maeneo ya kushirikiana ikiwemo kukuza utalii wa uwindaji na kutoa vifaa vya kukabiliana na  ujangili wa wanyamapori

Aidha, Katika mazungumzo hayo wamejadiliana  masuala ya Uwekezaji  ambapo Dkt.Ndumbaro amewaita Wawekezaji wa Marekani hususan Matajiri wa Jimbo la Dallas kuja kuwekeza Tanzani kwa kujenga mahoteli yenye hadhi ya nyota tano

Katika vikao hivyo vya Waziri Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani  nchini Marerkani  Dkt. Elsie Kanza pamoja na Ujumbe wa kutoka Tanzania akwemo Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jenerali, Hamisi Semfuko, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi na Afisa Mwandamizi, Segoline Tarimo

No comments:

Post a Comment