Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoni Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani Copro Steven Mchomvu kwa kupokea rushwa eneo la Ipogolo manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa mkoni Iringa imethibitisha kumkamata askari wa usalama barabarani kwa
kosa la kupokea rushwa kwenye mabasi maeneo ya Ipogolo manispaa ya Iringa tarehe
18/01/ 2022.
Akizungumza na waandishi wa
habari mkoani Iringa kamanda TAKUKURU mkoa wa Iringa,Domina Mukama alisema kuwa
walimukamata Copro Steven Mchomvu akipokea rushwa kwenye mabasi ambayo yanapita
katika barabara ya ipogolo.
Alisema kuwa picha ambazo
zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zilipigwa na maafisa wa TAKUKURU mkoa wa
Iringa mara baada ya kumkamata askari huyo wa usalama barabarani akipokea
rushwa kutoka kwenye basi.
Mukama alisema kuwa polisi huyo
bado anashikiriwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa na taratibu zote
zikikamilika atapelekwa ndio watatoa taarifa nini kitafanyika kwa mujibu wa
sheria za nchi.
Alisema kuwa walimkuta na kiasi cha shilingi laki moja na nusu pesa tathilimu ambazo alikuwa nazo mfukoni ambazo alikuwa akipokea rushwa kwa magari mbalimbali
Alitoa onyo kwa watumishi wote
wa serikali waache mara moja tabia ya kutoa na kupokea rushwa kwa kuwa ni
kinyume cha sheria za utumishi wa UMMA kama ambavyo walikula kiapo wanapoanza
kazi.
Mukama alisema kuwa mara baada
ya kumkamata askali wa usalama barabarani copro Steven Mchomvu alimshirikisha
OCD wa Iringa kwa sababu vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa
pamoja.
Aidha kamanda wa TAKUKURU mkoa
wa Iringa alisema kuwa wamefanikiwa kukagua jumla ya miradi kumi na mbili (12)
yenye thamani ya shilingi bilioni saba milioni mia moja themanini na tano elimu
mia tano sabini na tisa na kumi na tano (7,135,579,015).
Alisema kuwa miradi hiyo ni ya
sekta ya elimu,ujenzi (barabara) na afya ambayo miradi hiyo ilikaguliwa kwa
lengo la kujua thamani halisi ya pesa iliyotumika na na ubora wa miradi husika
kama inaendana na miradi yote ilikaguliwa na kukuta inaendelea vizuri na kwa
ubora unaotakiwa.
Mukama alisema kwa kipindi cha oktoba na disemba mwaka 2021 walipokea jumla ya malalamiko 48 yanayohusiana na rushwa lakini baada ya uchunguzi waligundua kuwa taarifa za rushwa zilikuwa 26 na 22 hazihusiani na rushwa.
No comments:
Post a Comment