Thursday, January 13, 2022

Mwandishi Global TV Arusha Aukimbia U-Spika, Atangaza kujipanga kugombea Jimbo la Kongwa

 

Pichani:Aliyekuwa Mtangazania wa Ubunge Jimbo la la Arusha Mjini 2015 kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Korumba Lebabaz ( Mwandishi Msomi)Picha na Innocent Natai


Na Innocent Natai

Aliyekuwa Mtangazania wa Ubunge Jimbo la la Arusha Mjini 2015 kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Korumba Lebabaz ( Mwandishi Msomi) ambaye pia ni mwandishi wa habari kutoka kituo cha Global Tv Nchini Tanzania ameweka wazi swala la kuto kugombea nafasi ya U-Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lebabaz ameyasema hayo Leo Janyari 12,2022, alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari Jijini Arusha, ambapo ameleeza kwamba kilicho mpelekea hadi kutokuchukua fomu za kutikugombea nafasi hiyo ya U-spika kwa kupitia chama chake cha mapinduzi (CCM) ni kutokana na watangulizi wake waliyochukua fomu hiyo kupitia chama chake ni kutokana na uwezo mkubwa waliyo nao watangulizi wake.

"Nimefikia uwamuzi hui ni baada ya kuona waliyo chukua fumo tayari kupitia chama changu cha mapinduzi wanazo sifa za kutosha na uwezo mkubwa wa kuliendesha bunge nimeona kujitoa na kuwaachia kuendelea na mchakato huo ambao natarajia utapata spika bora wa kuliongoza Bunge letu kwa kipindi hichi ambacho Nchini yetu inahitaji umahili mkubwa kwa viongozi kwa ustawi wa uchumi wa Nchi yetu". Amesema Korumba.

"Kwa swala la aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai siwelzi kuliongea sana ila niwashukuru wanachana na wanademokrasia waliyoweza kumshauri vyema Mhe Ndugai kwa ubapande wangu mimi ninaona bado ninayo nafasi ya kwenda kuwatumikia wanakongwa maana nimekaa sana kongwa na ninaimani kupitia chama changu ninaweza kupata nafasi ya kuwatumikia wanakongwa." Aliongeza Korumba Lebabaz.

Aidha Korumba alieleza sababu za yeye kuhamishia nguvu katika Jimbo hilo la kongwa ni kutoka na malezi yake hadi masomo yake kufanyia huko na sasa anaona anayo sababu ya kurudisha shukrani kwa wanakongwa kwa kuwatumikia.

"Nimesema elimu ya awali na msingi katika shule ya Ranchi ya Nako, elimu yangu ya Sekondari nimesoma Kibagwa Sekondari hadi kidato cha nne iliyo katika Jimbo hilo la kwangwa kabla sijaendelea na masome mengine ngazi za juu lakini hizi sio sababu tu za mimi kusema nikawatumikie wanakongwa ila nasubilia mpaka chama changu kitakapo fungua milango kwasasa siwezi kusema mengi nasubilia muda ufike." alosema Lebabaz

Aidha Lebabaz ameeleza kwamba bado zipo nafasi mbali mbali katika taifa hili kwa vijana wowote wazalendo wanatakiwa kuzichukulia kwa umakini ili kukuza ustawi wa uchumi kutokana kuwa na fikra chanya kwa kuwasaidia viongozi wa ngazi za juu.

"Najua wapo vujana wengi ambao wamepewa nafasi lakini wamezichezea sana na kuwakatisha tamaa viongozi pia wapo wazee wanaofanya vizuri tunatakiwa kuwasaidia vyema ili kujenga nyumba moja yenye maendeleo bora kwetu sote watanzania kikubwa tu viongozi wetu waendelee kutuamini kwa kila mmoja wetu kwafasi yetu." Ameongeza Lebabaz.


No comments:

Post a Comment