Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Watumishi wa Wizara yake wakati alipofika katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akifurahia jambo na Katibu Mkuu wake Dkt. Zainabu Chaula wakati alipopokelewa katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akisalimiana na baadhi wa Watumishi wa Wizara yake wakati alipopokelewa katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (wa pili kuliwla) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu wake Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ( wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula kulia na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara yake wakati alipopokelewa katika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa kushika nafasi hiyo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJWM
Na WMJWM Dodoma
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameahidi Utumishi uliotuka katika Wizara hiyo Mpya na kuhimiza suala la Umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi.
Dkt Gwajima ameyasema hayo wakati akizungumza na Menejimenti na watumishi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum katika Ofisi za Wizara matika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Amesema katika kuleta uwajibikaji wenye msukumo chanya tutahitaji kuwa na “Scorecard” Ili kupima uwajibikaji wa kila mmoja kwa ajili ya kupata matokeo ya haraka na kufikia kwa haraka zaidi matarajio ya Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyewezesha kuanzishwa wa Wizara hii muhimu kwa maendeleo na ustawi wa taifa letu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis ameahidi kutoa ushirikiano Mkubwa kwa Waziri Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na watumishi wote wa Wizara ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na ustawi wao.
Awali akizungumza katika.hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainabu Chaula amemuhakikishia Waziri Gwajima kuwa atasimamia wakurugenzi na watumishi sambamba na kutumia utaalam wao katika kuwezesha Wizara katika kuleta matokeo chanja kwa wananchi.
Akisalimia kwenye hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju amesema jukumu la kuleta Maendeleo kwa wananchi ni pana na Wizara wezeshi, hivyo lazima uwepo na ushirikiano na Wizara na wadau wengine utasaidia kuletea wananchi Mamaendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Patrick Golwike amemuakikishia Waziri kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika kutimiza lengo lililokusudiwa na Rais katika Wizara hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Januari 08, 2022 aliwateua Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima na Naibu wake Mhe. Mwanaidi Ali Khamis, Dkt. Zainab Chaula kuwa Katibu Mkuu akisaidiwa na Naibu Katibu Mkuu Amon Mpanju viongozi ambao waliapishwa rasmi tarehe 10 Januari, 2022 kuiongoza
No comments:
Post a Comment