Wednesday, January 12, 2022

KAMATI YA MRADI WA KOROSHO MANYONI YAPEWA MAAGIZO MAZITO, YADAIWA KUPOKEA ZAIDI YA MILIONI 600 ZA MASHAMBA YA KOROSHO.



Mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenga akizungumza na wajumbe wa kamati ya mradi wa korosho wilaya ya manyoni akiwa ameambatana na  Bi Rahabu Mwagisa mkuu wa wilaya ya manyoni alieko kulia na Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya manyoni Melkzedeki Humbe .

 


Baadhi ya wajumbe wa kamati ya mradi wa korosho wakiwa katika kikao na mkuu wa mkoa wa singida , kushoto ni fadhil chimsala afisa kilimo wilaya ya manyoni.


Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya wilaya ya Manyoni Aderaide Rweikiza akitoa taarifa mradi wa kilimo cha korosho na Hali halisi ya ugawaji wa mashamba ya korosho kwa watu waliolipia fedha .


Mkuu wa wilaya ya Manyoni Rahabu Mwagisa akitoa maelekezo ya namna ya kutatua mgogoro utokanao na mashamba ya korosho ambapo imedaiwa kuwa zaidi y ash. Milioni 600 zimetoka kwa watu kwaajili ya kununua mashamba hayo.


Na Hamis Hussein - SINGIDA

KAMATI ya mradi wa kilimo cha korosho kutoka halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani hapa imetakiwa kutoa taarifa ya kina kufuatia madai ya  kupokea zaidi ya Sh.milioni 600 kutoka kwa watu 180 kutoka ndani na nje ya nchi  ambao waliahidiwa kuwapatia mashamba ya kulima korosho lakini hawajagawiwa maeneo hayo ikiwa ni miaka minne sasa.

Kufuatia malalamiko ya watu waliotoa fedha hizo kwa kuziweka kwenye akaunti maalumu ya halmashauri kama walivyokuwa wameelekezwa, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Binilith Mahenge aliitisha kikao cha kamati tendaji ya mradi wa korosho Manyoni na amesema amepokea orodha ya watu 180 kutoka ndani na nje ya nchi wakilalamikia kutopata mashamba hayo na pesa tayari walishatoa.

Kikao hicho kilicho wakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wale wa kilimo , wataalamu kutoka idara mbalimbali, viongozi wa halmashauri ya manyoni , mkuu wa wilaya hiyo  Bi. Rahabu Mwagisa pamoja na mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge kililenga kutafuta suluhu ya mgogoro huo wa mashamba ya korosho ambao umekuwa kwa muda sasa na kupitia kikao hicho ,Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa aligiza kufungwa akaunti zote za kupokea fedha za ununuzi wa mashamba hayo hadi utakapofanyika uhakiki wa kujiridhisha.

Sanjari na hilo Mkuu wa Mkoa Dk.Mahenge aliiagiza kamati hiyo hadi kufika Jumatatu ya Januari 17 mwaka huu iwe imetoa taarifa ya mradi huo iliyosahihi ambayo itapitiwa na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS) Mwalimu Doroth Mwaluko  kabla ya kuwasilishwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa.

Kando ya agizo hilo pia Dkt.Mahenge aliwataka kuandaa upya na  kufuatia taarifa iliyokuwa ikitolewa kutojitosheleza kwani majina ya baadhi ya watu wanaodaiwa kulipia fedha hayakuwepo licha ya yeye kuwa nayo huku kiasi cha fedha kilichopokelewa kikiwa hakijabainishwa.

"Taarifa hiyo muiandae vizuri najua hizo namba mnazo nendeni mkaziunganishe na muwe makini kama kuna watu walikuwa wakiingiza fedha hizo benki mnapaswa kuwajua, wapo walioleta fedha hizo ofisini, mliowapa mashamba, ambao bado hamjawapa, waliopanda au kupalilia hivyo nawaombeni tengenezeni taarifa inayojitosheleza," alisema Dkt. Mahenge.

Mkuu huyo wa mkoa wa singida mwenye uzoefu mkubwa wa utendaji serikalini  aliostajabishwa namna kamati hiyo ilivyokea fedha za watu kwaajili ya mashamba hayo na watendaji wake wasiwe na taarifa sahihi.

"Haiwezekani mkapokea fedha za mtu halafu mkashindwa kuandaa taarifa kwani jambo hilo sio geni kwao na kama taarifa hiyo inashindwa kuandaliwa vizuri patakuwa na kizungumkuti hamna taarifa hizo huenda zitakuwa kwa mtu mmoja bila kushirikishwa wengine na hawajui lakini kama wajumbe wote wa kamati hiyo wangekuwa wanajua isingeshindwa kuandaliwa” Alisema Dkt. Mahenge  katika kikao hicho .

Licha ya kutoa agizo kwa kamati ya korosho mkoa wa singida hususani katika halmashauri ya Manyoni Dkt. alitaka changamoto hiyo waimalize na kuwa jambo hilo anamuachia mkurugenzi na lifanyike chini ya Katibu Tawala na sio kuiachia kamati hiyo peke yao na kuwa kama watashindwa kupata mzani waende kwenye hayo mashamba kujiridhisha kwa kuhakiki majina ya wamiliki wa mashamba hayo.

Alisema taarifa  mpya watakayoitoa baada ya kuipitia kwa makini inapaswa  ioneshe fedha zilizopokelewa na mashamba yake  huku akionesha wasiwasi kuwa  kuna uwezekano wa fedha zilizoingizwa zikawa ni zaidi ya  ekari za mashamba walizonazo hivyo waeleze kuwa kutokana na kutofunga akaunti walipokea fedha hizo ili kama kutakuwa na uwezekano watu hao ambao watakosa maeneo watafutiwe sehemu nyingi kama Itigi au Ikungi kwa makubaliano kwa sababu shida yao ni kupata mashamba.

Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Manyoni ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo Aderaide Rweikiza  alisema mradi huo wa korosho mkoani singida ulikuwa ni matokeo ya andiko lilikuwa limeanisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kupitia andiko hilo liliambana na utafiti kuwa wilaya ya manyoni ndio inaweza kuzalisha korosho kwa mkoa wa singida hivyo mchakato ukaanza mwaka 2017  kwa kuwashirikisha wakulima kwa kuwagawia ardhi kwa bei elekezi.

“Ulipendekezwa mradi wa korosho ukaoneka kuwa unaweza kulimwa manyoni , mheshimiwa mkuu wa mkoa mwaka 2016 tulipeleka andiko letu  lakini tukaona kwamba andiko bado halija kamilika tukaona  tusiombe mkopo , tukaona tukalibishe wakulima ambapo wanaweza kuwa kwenye mradi wetu na tukaona wakulima wachangie” alisema mkaguzi wa ndani wa halmashauri ya manyoni .


No comments:

Post a Comment