Wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa jukwaa la pili lililofanyika January 14 mkoani singida.
Mkurugenzi wa Rasilimali za maji Dkt. George Lugomela akitoa hutuba wakati akimwakilisha katibu mkuu wizara ya maji katika kikao cha jukwaa la maji bodi ya maji bonde la kati mkoani singida.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa singida Alhaji Juma Kilimba akiwa katika kikao cha jukwaa la wadau wa maji bodi maji bonde la kati ilifanyika katika ukumbi wa Bodi ya maji bonde la maji zilizopo mkoani singida.
Baadhi ya washiriki wa jukwaa la pili la wadau maji wa bodi ya maji bonde la kati wakifuatilia mada mbalimbali zikitolewa wakati kikao kikiendeelea .
Na Hamis Hussein – Singida
WADAU wa jukwaa la maji bodi
ya maji bonde la kati wameitahadharisha jamii kutunza na kumia vizuri maji na
vyanzo vyake ili viwasaidie hapo baadae kwa kuna kunauwezekano wa kutokea kwa uhaba wa maji kutokana na uchache
wa mvua unaoendelea katika maeneo
mbalimbali ambao ndio chanzo kikuu cha asili ya maji.
Wadau hao wa maji wa bodi ya maji bonde la kati
wakiwa katika Kupitia jukwaa la pili lililolenga kuandaa na kuidhinisha
mipangokazi ya vikundi kazi , pamoja na
mambo mengine wameisisitiza jamkii kutumia vizuri maji pamoja na kutunza vyanzo
vya maji katika maeneo kwani uchache wa mvua uliojionyesha msimu huu unatishia
kuwepo kwa kiwango cha maji ya kutosha ambapo mwenyekiti wa bodi za maji za
mabonde nchini ambaye pia ni mkurugenzi
wa bodi maji bonde la pangani Segule Segule amesema licha ya uchache wa maji
uliopo hivi sasa jamii pia inapaswa kutumia vizuri maji
“ Hali ya maji kwa ujumla wake iko vizuri lakini kuna pahala pamekosa
kidogo pengine pamepungua , sisi kama watu wa maji tunachokifanya tuanendelea
kuhimizana watumie kidogo kidogo watambue kuwa kipindi cha ukame kimejitokeza
sasa ” Alisema Segule Mwenyekiti wa Bodi za maji za mabonde nchini
Aliongeza kuwa kama serikali
kupungua kwa maji inatoa ishara ya kutengeneza miundombinu ya kutunza maji kwa ujenzi wa mabwawa na miundombinu ya
kuifadhia maji kutokana maji mengi ya
asili yatokanayo na mvua yanaenda kwenye maziwa
na mengine yanapotea .
Afisa maendeleo ya jamii
mwandamizi wa bonde la kati Bi Nelea Bundala amesema hali ya maji kwa bonde
hilo sio nzuri na huwenda ikasababisha migogoro ya maji kutokana nauhalibifu wa
miondombinu ya maji kutokana asili ya jamii hiyo ambayo asilimia kuwa ni ya
wafungaji .
“Mwishoni mwa 2021 mpaka hapa tulipofikia hali za rasilimali ya maji nchini sio
nzuri hususani bonde letu la kati tuna
mikoa nane , mikoa hiyo ipo katikati ya nchi na inaongoza kwa idadi ya mifugo
nchini asilimia 58 ya mifugo nchini inayopatikana na ukiangalia athali za
kwenye vyanzo vya maji , ukame unazidi mabadiliko ya tabia nchi hali imeathiri
vyanzo vya maji , mifugo imeanza kufa na
hali hii kama itaendelea hivi itaweza kuleta migogoro ya matumizi ya maji ”
alisema Nelea Bundala Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi bodi ya maji bonde la kati .
Bi. Nelea Bundala Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi bodi ya maji bonde la kati akielezea hali halisi ya upatikanaji wa maji kwa kipindi hiki cha ukame.
Mwenyekiti wa Bodi za maji za mabonde ambaye pia ni Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la pangani Segule Segule Akitoa tahadhari ya kutumia maji vizuri pamoja na kutunza vyanzo vya maji kutokana na tishio la ukame msimu huu aliposhiriki katika jukwaa la pili la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati mkoani singida.
Lazaro Msagu Mwenyekiti wa jukwaa la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati Akitoa Ushauri wake kwa wanajukwaa kufanya tathmini ya namna ya kutafuta suluhu kulikomboa bonde hilo.
Hata hivyo Bi Nelea hakuishia
hapo akataoa wito na pendekezo kwa wadau wote wa maji kupitia idara mbalimbali
kutoa elimu kwa jamii namna ya kutunza vyanzo
vya maji ili viweze kusaidia katika kipindi hichi ambacho kuna tishio la
ukame .
Kupotea au kupungua kwa maji
katika maeneo mbali mbali kunachagizwa na
shughuli za kibinadamu kama vile kulima ndani ya vyanzo vya maji ,
uchenjuaji wa madini , utifuaji wa ardhi
nakadhalika Kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati danford
Samson alitaja shughuli za hizo za binadamu zinavyoharibu vyanzo vya maji na
kupelekea ukame.
“Upungufu wa sahivi unasababishwa na shughuli za kibinadamu kulimo
ndani ya mita 60 , kufanyatua tofali kwenye mito , uchenjuaji wa madini hasa dhahabu mwenye vyanzo vya maji kama vile
mito au ziwa” . Alisema Danford .
Kaimu MKurugenzi wa bodi ya maji bonde la kati Danford Samson Akifafanua baadhi ya mambo kwa waandishi wa Habari.
Wanajukwaa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa kwenye jukwaa la pili la pili la wadau wa maji wa bodi ya maji bonde la kati
Mkurugenzi wa Rasilimali Za Maji
Dkt. George Lugomela akimwakilisha katibu mkuu wa wizara ya maji alisema jukwaaa la wadau wa bodi ya maji linapaswa
kuunda majukwaa mengine madogo katika maeneo yao ya ngazi ya chini ili kurahisisha utatuzi wa changamoto za bonde
la kati sanjari na kuwavutia wadau.
“Tunatakiwa tuendelee kuzindua majukwa ya bonde madogo ya maji au
vidaka maji (catchment) hatuatikiwa kuishia kwenye mabonde ya kanda au la
taifa tuwende kwenye mabonde madogo mfano hapa kwenu mna mabonde madogo nane ziwa easi , natron maana yake changamoto za easi na natron
zitakuwa tofauti na mtaweza kujadiliana”. Alisema Dkt. Lugomela
Mwenyekiti wa jukwaa la wadau wa
maji bodi maji bonde la kati lazaro
msagu amesema wao kama wadau wanapaswa kufanya tathmini ya namna ya kutatua
changamoto za maji katika bonde hilo la kati
Kwa mujibu wa jukwaa la wadau wa
maji bodi ya maji bonde la kati zaidi ya
watu 200 wa bonde la kati wana maji lakini
hawana vibali vya kutumia
rasilimali hiyo jambo ambalo jukwaa limepaswa kuitatua changamoto hiyo .
Jukwaa la wadau wa maji bodi ya maji bonde la kati liliundwa mwaka 2019 mara baada ya kuanzishwa kwa jukwa la wadu wa maji ya bonde la taifa 2017 ambapo katika kikao cha janury 14 mwaka huu kilijikita kuangazia majukwa mengine yaliopita sanjari na kupendekeza wajumbe wa bodi ya maji bonde la kati ambao wataenda kuchaguliwa na waziri wa maji.
No comments:
Post a Comment