Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa juu ya kuachana na biashara ya ngono na wafuate kilichowapeleka chuoni.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akikabidhiwa zawadi na Rais wa chuo kikuu cha Iringa (Tumaini) Elius wiliam baada ya kufika chuoni hapo kwa mara ya kwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa juu ya kuachana na biashara ya ngono na wafuate kilichowapeleka chuoni.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema tabia ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Iringa Kujihusisha na Biashara ya Ngono kunadharirisha Utu na hadhi ya Vyuo,elimu wanayoipata na hilo sio kusudio la serikali.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo Kikuu Iringa (Tumaini) alisema Serikali imebaini kuwapo kwa wasichana wanaofanya biashara hiyo haramu huku akionya kuchukua hatua.
Moyo alisema kuwa serikali inawategemea wasomi wa Elinu ya juu kuwa chachu ya maendeleo kwa kufanya tafiti zenye tija na kuishauri serikali Juu ya masuala ya maendeleo, na si kujihusisha na vitendo vya aibu
Alisema kuwa tatbia hiyo inachafua taswira ya elimu ambayo inatolewa na vyuo vikuu vya mkoani Iringa kwasbabu ya wanafunzi wachache ambao wamejikita katika biashara hiyo ya ngono.
Moyo alionyesha kukerwa na vitendo vya baadhi ya wanachuo kwa tabia zao za kujihusisha na biasha ya Ngono lakini anavitaja vitendo hivyo vinaondosha thamani ama hadhi ya elimu ya vyuo vikuu na kuchafua taswra halisi ya elimu hiyo ya juu
“Ukipita kwenye kumbi mbalimbali za starehe nyakati hasa za siku unakutana na wimbi kubwa la baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wapo wanadanga tu bila sababu yoyote ya msingi hivyo wanafunzi wanatakiwa kuacha mara moja tabia hiyo ya udangaji” alisema
Alisisitiza kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaosoma vyuo vilivyopo mkoani Iringa kuachana na tabia zisizo na tija na badala yake sasa wajielekeze katika uzalendo wa kweli kwa Taifa.
Moyo alisema kuwa serikali imekuwa inatoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa lengo la kuwasaidia kutimiza majukumu yao yaliyowapeleka vyuoni na sio fedha hiyo waitumie kwenye starehe kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakifanya.
Alilazimika kuyasema hayo kutokana na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati kuwatumia vijana wa vyuo vikuu nchini kuichafua serikali kwa kuwakashifu viongozi waliopo madarakani na kupinga masuala ya maendeleo pasipo kupima athari zinazoweza kujitokeza kwa Taifa
Moyo alisema kuwa biashara ya ngono inamadhara makubwa kwa wanafunzi kwa kuwa wanaweza kupata mimba na magonjwa mbalimbali ambayo yatasababisha kutisha ndoto zao za kupata elimu ya juu.
Kwa upande wake rais wa chuo kikuu cha Iringa (tumaini) Elius wiliam alisema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa chuo hicho juu ya madhara yanayotokana na biashara ya ngono ambayo baadhi ya wanafunzi wanakuwa wanaifanya.
Wiliam aliwataka wanafunzi wa chuo hicho kuyaishi maisha ya chuo kwa kangalia ni kilicho wapeleka kufika chuoni ili wafikie malengo ya na akasema kuwa starehe zipo tu haziishi duniani hivyo watimize kwanza malengo ndio wafanye mambo mengine.
Naye makamu mkuu wa chuo kikuu cha Iringa Profesa Ndelilio Urio alimushukuru mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kuwafunda wanafunzi hao kwa maswala mbalimbili ikiwepo wa madhara ya bishara ya ngono kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment