Monday, January 24, 2022

CCM SINGIDA YAIUNGA MKONO HALMASHAURI KUU TAIFA KUMTEUA DK. TULIA AKSON KUGOMBEA USIPIKA

 


 


Mkuu wa mkoa wa singida Dkt. Binilith Mahenge wapili kutoka kushoto , Mwenyekiti wa ccm mkoa wa singida Alhaj Juma Kilimba wapili kutoka kulia , Yohana msita Mjumbe wa halmashauri kuu taifa kwa mkoa  wa kwanza kulia na singida Lucy Boniface katibu wa ccm  wa kwanza kushoto wakiwa katika kikao cha halmashauri kuu ya chama kilichofanyika janury 22 mjini singida.

 



Mwenyekiti wa ccm alhaj juma kilimba akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya ccm katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa



Wakuu wa wilaya , wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali wakifuatilia kikao cha halmashauri kuu

 



Ndugu Francis Isaack (Mb) wa iramba mashariki akichangia kwenye kikao cha halmashauri kuu juu ya suala la ukopeshaji wa mbegu kwa wakulima.



Ndugu  Miraji Mtaturu (Mb) wa singida mashariki akichangia kwenye kikao cha halmashauri kuu ya ccm singida



Elia Digha mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida  akiuliza msimamo wa serikali juu ya utunzaji rasilimali za halmashauri hiyo.



Wajumbe wakisikiliza hoja zikitolewa kwenye kikao.

 

Na Nathaniel Limu - SINGIDA

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida kimempongeza mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Dk.Tulia Ackson kugombea nafasi ya spika wa Bunge kufuatia kujiudhuru kwa  aliyekuwa spika ndugu Job Ndugai.

Pongezi hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita  na kamati  kuu ya CCM mkoa wa Singida,kwenye kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika kipindi cha kuanzia julai hadi desemba mwaka jana (2021).

Kamati hiyo imesema uteuzi huo ni sahihi ikizingatiwa Dk.Tulia ana uzoefu wa muda mrefu   katika kuliongoza bunge kwa ufanisi mkubwa na kuwaomba wabunge wa singida walihudhuria kikao hicho kwenda kumpigia kura Dk Tulia ili aweze kuliongoza bunge tukufu.

“Ninyi wabunge wetu wa mkoani kwetu,nendeni mkatuchangulie kwa kura zote Dk.Tulia,ili ashinde kwa kishindo.Mteule wetu uwezo anao tena mkubwa tu.Imani yetu kwake ni kwamba atasimamia bunge kikamilifu, ili muhimili huo utekeleze majukumu yake kwa ufanisi”,amesema Alhaj Kilimba.

Kwa upande wa ilani ya uchaguzi,mwenyekiti huyo alisema chama kinaipongeza serikali ya mkoa wa Singida chini ya uongozi thabiti wa mkuu wa mkoa Dkt.Binilith Mahenge Kwa utekelezaji wake wa ilani ya uchaguzi kwa kiwango kilichokusudiwa.

Akifafanua,alisema kuwa katika miradi yote ya sekta mbalimbali iliyotembelewa na kamati za siasa za wilaya na mkoa,miradi hiyo imetekelezwa kama ilivyokusudiwa.Na ina thamani ya fedha zilizotumika.

“Miradi kama ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari,ipo vizuri sana na inavutia.Hongereni sana, na kipekee pongezi nyingi ziende kwa mkuu wa mkoa Dkt.Mahenge”,amesema mwenyekiti huyo.

Pia Alhaj Kilimba,alitumia nafasi hiyo kumshukru Rais Samia kwa uamuzi wake wa kuupatia mkoa wa Singida, fedha nyingi zilizotosha kugharamia miradi mbalimbali.

”Sisi wasaidizi wako na Watanzania kwa ujumla,tutaendelea kukuombea kwa Mwenezi Mungu akupe nguvu na afya njema, ili uendelea kuwatumikia vema Watanzania wenzako”.aliongeza alihaji kilimba  mwenyekiti ccm singida

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Singida,Dkt.Mahenge alisema kuwa katika kipindi hicho,mkoa umepokea zaidi ya shilingi 13.4 bilioni kupitia UVIKO-19 kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa 330 kwa shule za sekondari na 332 vya shule za msingi.

Alisema vyumba  hivyo vya madarasa vimekamilika kwa wakati na  vina viti,meza na  madawati ya kukidhi mahitaji .

“Katika kipindi cha utekelezaji ,mkoa umepokea jumla ya shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ukarabati,upanuzi na ujenzi wa miundo mbinu mbali mbali katika vituo vya afya 11 kupitia tozo”,alisema mkuu huyo wa mkoa.

Dkt.Mahenge alisema pamoja na mafanikio mengi waliyopata katika kipindi hicho,vile vile walikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa watumishi, kuchelewa kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi wa miradi ya elimu na bei ya bidhaa kupanda.

Naye katibu tawala mkoa wa Singida,Doroth Mwaluko,ameahidi kabla ya jumatano wiki hii,taarifa juu ya stofahamu ya fedha zaidi ya 660 milioni za zao la korosho,itakuwa imefahamika.

Wakati huo huo,katibu CCM mkoa wa Singida,Lucis Boniface,alisema katika miradi yote mkoani waliyoikagua,hawajapata dosari yo yote.Amewapongeza wakuu wa wilaya ya watendaji wengine waliosimamia miradi hiyo.

Aidha,alisema ujenzi wa daraja la Misingi wilaya ya Mkalama,kazi inaendelea vizuri.Kamati ilitatua mgogoro wa ujenzi wa kituo cha afya Mkalama, na sasa kazi ya ujenzi wa kituo hicho inaendelea.

Awali kikao hicho kilisimama kwa dakika moja,kumkumbuka na kumwombea mwalimu sekondari Luluma wilaya ya Iramba,Simon Anthony, aliyeuawa na mke wake Mwanaisha  Shamiru,kwa kuchomwa moto.

 

No comments:

Post a Comment