Thursday, December 9, 2021

Dc Kasulu Kanali Isaac Mwakisu aongoza kusheherekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi Kasulu mjini.

 








Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu leo ameongoza Viongozi wa Serikali, Chama, Taasisi mbali mbali  pamoja na Wananchi kusheherekea miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania kwa kufanya usafi Kasulu mjini.

 Aidha pia Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu aliongoza upandaji wa Miti 1200 katika eneo la Mkuu wa Wilaya sambamba na Vyombo Vyote vya Ulinzi na Usalama huku akitoa Pongezi kwa Serikali kwa namna inaleta Maendeleo. Aliwatakia Watanzania wote na Wananchi wa Kasulu heri ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania .

Ambapo REDESO ndio waliotoa Miche 1200 ambayo inaweza kupandwa kwa ajiri ya Kilimo Mseto ( Agroforest ) aina Miche iyo ni Grevilea, Robusta, Maesopsis Emini (Mibamula) Mikangazi : Khaya anthotheca. Miti ya Kiasiri ni thamani ya Mbao pia ina rutubisha Ardhi.

No comments:

Post a Comment