Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Burian akiwa anamkabidhi mfuko wa Mbegu za Alizeti kaimu mkurungezi wa manispaa ya Tabora Seif Salum kwenye kituo cha Reli Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Burian akiwa ameshikilia mfuko wa Mbegu ya Alizeti pembeni yake mkono wa kushoto aliyafaa suti ni Afisa Masoko wa Asa Emmanuel Luoga na katika ni katibu msaidizi huduma za Kilimo Raphael,Nyanda
Na Lucas Raphael,Tabora
Mkoa wa Tabora umepokea shehena tani 116 za mbegu za alizeti ikiwa ni mapokezi ya awali kati ya tani 240 ambazo ni kwa ajili ya msimu wa Kilimo wa mwaka 2021-2022
Alizeti hiyo ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa Serikali wa kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula nchini ambao umeelekezwa kutatuliwa kupitia kilimo cha alizeti.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dr.Batilda Burian alisema kwamba kufika kwa shehena hiyo ya Mbegu za alizeti kutoka Wakala wa mbegu nchini ASA itawasaidia wakulima mkoani humo.
Mkuu huyo wa mkoa wa Tabora alipokea shehena hiyo jana kwenye Kituo cha reli ya kati mkoani Tabora kutoka kwa Wakala wa Mbegu nchini ASA .
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dr.Batilda Burian anakiri Shehena hiyo ya Mbegu za alizeti itasaidia kwenye kilimo kufikia lengo la kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kula nchini
Hata hivyo aliwaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi kusimamia mbegu hizo ili ziweze kuleta tija.
Awali afisa masoko wa wakala wa mbegu nchini kutoka mkoa wa shinyanga Emmanuel Luoga akizungumza kabla ya kukabidhi shehena hiyo alisema kwamba mkulima akilima Mbegu hiyo inauzao wa kumpatia magunia kati ya gunia 7 hadi 11 zenye ujazo wa kilo 60 kwa ekari kulingana na huduma itakayotolewa wakati wa uzalishaji wake.
Aliendelea kusema kwamba wakulima walime mbegu hiyo kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuwahakikishia mavuno bora ambayo yataongeza upatikanaji wa mafuta mengi ya alizeti nchi.
Alisema kwamba wakala alipokea mahitaji ya mbegu za alizeti (Standard seeds) kwa mkoa wa Tabora zaidi ya tani 208 Kwa kuanzia ASA wamekabidhi tani 116 kati ya mahitaji yaliyoombwa.
Katika msimu huu wa 2021/22, Wakala wa Mbegu za nchini ASA umepokea maelekezo ya Wizara juu ya maandalizi na usambazaji wa zaidi ya tani 2000 za mbegu ya alizeti inazotarajiwa kuwafikia wakulima katika maeneo mbalimbali nchini ili kuwahi msimu wa Kilimo.
Serikali ilionesha Maeneo yakipaumbele katika halmashauri za mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Simiyu na Tabora.
No comments:
Post a Comment