Na Chifu Ahmed Missanga Senge
Leo Tarehe 17.11.221 imekuwa baraka Ihanja wilayani Ikungi katika Mkoa wa Singida kusimikwa ramsi Chifu Singu Missanga Senge Kuwa kiongozi wa Utemi wa UNYIKUNGU katika kabila la Wanyanturu. Hafla ya usimikwaji zilianza kwa Dua maalum ilioyo ongozwa na viongozi mbalimbali wa dini Shekhe , Mchungaji kisha Dua ya kimila ya Wanyaturu. Chifu Singu Missanga amesimikwa na baraza la wazee la ukoo wa Chifu Missanga Senge katika kabila la Wanyaturu na kushuhudiwa na Chifu mkuu wa Ikungi Abraham Gwau.
Akimwakilisha Jerry Muro Mkuu wa wilaya wa Ikungi, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Dijovison J. Ntangeki amesisitiza Viongozi wa Kimila kuwa ndio nguzo ya Amani na uwajibikaji hivyo watumie nafasi hizo kusaidia kuelelimisha jamii kuacha Mila potofu, kuhamasisha jamii kuenzi mila na tamaduni za Tanzania. Ikiwemo uhamasishaji upendo, maridhiano, umoja na mshikamano wa taifa ikienda sambamba na kulingania tunu za taifa pamoja na upendo ili kuondoa ukiukwaji wa Hali za binadamu wenye vionjo vya ubaguzi pia utunzaji wa mazingira ya asili, upandaji miti kwa wingi,kuhamasisha shughuli, za maendeleo , kilimo , ufugaji na uchapa kazi
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo Ni Afisa Tarafa wa kijiji cha Ihanja , Mhe. Madiwani, wenyeviti serikali ya vijiji na watendaji wa kata zote .
No comments:
Post a Comment