Tuesday, October 26, 2021

TANZANIA BILA DIRA YA MADINI


Ms. Jesca Kishoa, Mbunge.

Jana 25 October nilikuwa moja ya waalikwa katika mjadala uliolenga kuboresha hali ya sekta ya MADINI nchini. Pamoja na mchango wangu wa jana, nimekusudia kuweka nyongeza ya mchango wangu huo hapa. 👇🏽

Tanzania imepanga kuwa ifikapo 2025 sekta ya madini itachangia *10%* kwenye pato la Taifa (GDP), serikali imetumia miaka 5 kukuza sekta hiyo kutoka *3.8%* mwaka 2014/15 mpaka *5.2%* ambayo ni sawa na mapato ya Tsh. Billion *528.23* ya 2019/20. Ni miujiza gani itatumika kufikia lengo hilo la *10%* kwa miaka *4* ijayo?   

Pamoja na jitihada nyingine zote ikiwemo marekebisho ya sheria za madini na kanuni; *Mining Act of 2010 (revised edition 2018),* Tanzania Mineral Commission established under section 21 of written laws (Miscellaneous amendments no. 7) 2017, Natural Resource (Permanent Sovereignty act) 2017, Tanzania Extractive Industries (Transparency and Accountability) Act of 2015 na nyingine, bado hali ya mapato haiendani na thamani ya madini, bado loyalties ni single digit ( *6%* ) tu. 

Tanzania ni miongozi mwa nchi *54* zilizoshiriki na kusaini makubaliano ya Africa Mining Vision *(AMV)* *2009* . Dira hii ya madini barani Afrika ilitokana na kikao kazi cha mawaziri wa madini waliokutana na 2008, na februari 2009 andiko lilipata ukubalifu wa Umoja wa Afrika na kutambulika kama mongozo wa maboresho ya sekta ya madini Afrika, na kujikomboa toka kwenye ya uziduaji wenye mtazamo wa kinyonyaji, kuongeza uwazi na nchi kuwa na umikili wenye manufaa. Hii ni pamoja na kila nchi mwanachama kuwa na dira ya madini nchi yake *(CMV)* . 
Japo ni nchi *24* tu zilizoanza kuhuisha na kutekeleza tamko hili ya AMV kwa kuwa na CMV, mfano ni Kenya, Mali na Ghana, na nchi ya Lesotho pekee imefanikiwa kukamilisha kwa ufanisi. Nigeria imeshapata mafanikio kutokana na mwitikio wa dira hii, sasa itakuwa nchi itakayouza saruji katika mataifa mengine. 

Mara zote, Tanzania imekuwa na tatizo la kukubali na kusaini mikataba ya kimataifa lakini inachelewa sana kwenye utekelezaji, mifano ni kama hiyo ya Takwimu za COVID huko *WHO* , mikataba, protocol na makubaliano mbalimbali ikiwemo ya kikanda, bara na dunia. Ili kupunguza changamoto za sekta hii;
 *NAPENDEKEZA* 👇🏽
 *i* . Serikali iunde kamati na itenge bajeti ya utekelezaji wa tamko la AMV, ili tuwe na andiko la Dira ya Madini ya Taifa (CMV) itakayozingatia vipengele (clusters/principles) vyote vya AMV na kuihuisha (domesticate).

 *ii* . Wadau wa maendeleo wahusishwe kwenye kupanga vipaumbele 

 *iii* . Uwazi wa taarifa ya mapato na mikataba ya madini ni muhimu

 *iv* . Kujenga uwezo wa wazawa kupitia mpango wa Local Content 

 *v* . Serikali itenge bajeti ya Tafiti na mafunzo

 *vi* . TEITI iendelee kupewa rasilimali za kutosha ili kuendeleza ufanisi.

No comments:

Post a Comment