Aidha imesema zipo Jumuiya nyingine ambazo usajili wao
utafutwa kwa mujibu wa sheria endapo hawatoshiriki katika zoezi hilo huku ikivitaka vyama na vikundi vyote vyenye
sifa ya kusajiliwa kufika ili wapewe utaratibu wa kusajiliwa.
Agizo hilo limetolewa na Ndg. Emmanuel Kihampa Msajili Wa
Jumuiya, Wizara Ya Mambo Ya Ndani Ya Nchi Oktoba 22, 2021 Jijini Mwanza Wakati
akizungumza ndani ya kipindi cha Morning Express kinachorushwa na Kituo cha
Radio City fm 90.5 Mwanza kuhusu zoezi la kuhuisha vyeti vya Jumuiya zisizo za kidini kwa Mikoa ya Kanda
ya Ziwa.
Amesema ofisi yake
ilianza kazi tangu mwaka 1955 na ndiyo wenye dhamana ya kusajili Makanisa,
Misikiti na taasisi na mashirika ya kidini, vyama na vikundi vyote vya kijamii
na hivyo wameamua kusogeza huduma zao kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kupunguza
safari ya kufata huduma hiyo Mkoani Dodoma .
Akitolea mfano wa Jumuiya zisizo za Kidini Kihampa amezitaja
kwenye makundi manne ambayo ni Jumuiya za Kitamaduni akitolea mfano vyama vya
kikabila, Jumuiya za kiuchumi ambazo zinajihusisha na shuhuli za kiuchumi mfano
bodaboda, wajasiliamali, Jumuiya za Kijamii vyama vya kusaidiana mfano vya kufa
na kuzikana na Jumuiya ya Kitaaluma ni zile za wanataaluma mfano mafundi simu
nk.
Akizungumzia Lengo la zoezi hilo Linaloendelea Mkoani Mwanza amesema ni kubaini uhai wa Jumuiya kwani
tangia mwaka 1955 mpaka kufikia mwezi Julai 2021 orodha ya Jumuiya zilizopo ni
9,868 lakini wakija kuangalia kwenye utekelezaji wa usaji wamebaini Zaidi ya
50% ya Jumuiya hazionekani.
“Lengo la pili ni kutaka kufahamu hizi Jumuiya ambazo
zipo zinajiendeshaje tutataka kuangalia
katiba wanazotumia , malengo yao na
taratibu za uendeshaji je unawapa sifa za kuendelea kubaki kwenye regista ya
usajili Wizara ya Mambo ya ndani au tayari wameshapotweza sifa na je malengo na
taratibu za uendeshaji yanaenda sambamba na sheria za Jumuiya na sharia
nyingine za nchi yetu.?” Amesema
“Malengo mengine ni kutaka kubaini kama hizi Jumuiya
zinazingatia kikamilifu masharti ya Usajili ambayo yanahusisha uandaaji wa
nyaraka, ulipaji wa tozo mbalimbali pamoja na mabadiliko ya uongozi sambamba na
maelekezo ya Katiba zao” Ameongeza.
Amesema zoezi la kuhuisha usajili wa vyama, vikundi na
taasisi kwa hapa Mwanza limeanza Oktoba
20, 2021 na litafika tamati Oktoba 28, 2021 na kwa wale wanaotaka kuhuisha wanatakiwa kufika na nyaraka zikiwemo cheti
cha usajili, taarifa za fedha, taarifa
ya mabadiliko ya uongozi, uthibitisho wa malipo ya ada pia watataka kuona
katiba na kanuni ambazo wanazitumia katika uendeshaji wa shughuli zao.
Amesema wale wote ambao hawatojitokeza kushiriki zoezi hilo hadi
kufikia Novemba 30 mwaka huu vyeti vyao vitakuwa batili na watashindwa
kuvitumia na wale wote ambao watahitaji maelezo na ufafanuzi Zaidi wanaweza
kupiga simu namba 0734 712744 au barua pepe rs@moha.go.tz
No comments:
Post a Comment