Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma na Katibu wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma Bwana Meshack Bandawe, akiongoza kikao cha pili cha Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa wizara zote kujadili maendeleo ya ujenzi wa ofisi za ghorofa za Wizara zinazojengwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali Dodoma.
Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara zote wakifuatilia maelekezo yanayotolewa na Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma na Katibu wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma Bwana Meshack Bandawe,(Hayupo Pichani) kuhusu utekelezaji wa Ujenzi wa ofisi za Wizara za ghorofa zinazojengwa kwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali Dodoma.
Bi. Teddy Njau Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa ujenzi wa jengo la ghorofa la Wizara hiyo wakati wa kikao baina ya Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bwana Meshack Bandawe,(Hayupo Pichani) na Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara zote wakati wa kujadili utekelezaji wa Ujenzi wa ofisi za Wizara za ghorofa zinazojengwa kwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali Dodoma.
Bi. Beatrice Patrick Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa ujenzi wa jengo la ghorofa la Wizara hiyo wakati wa kikao baina ya Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bwana Meshack Bandawe,(Hayupo Pichani) na Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara zote wakati wa kujadili utekelezaji wa Ujenzi wa ofisi za Wizara za ghorofa zinazojengwa kwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali Dodoma.
Calvin Ntilia Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa ujenzi wa jengo la ghorofa la Wizara hiyo wakati wa kikao baina ya Mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali Dodoma Bwana Meshack Bandawe,(Hayupo Pichani) na Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara zote wakati wa kujadili utekelezaji wa Ujenzi wa ofisi za Wizara za ghorofa zinazojengwa kwa awamu ya pili katika Mji wa Serikali Dodoma.
No comments:
Post a Comment