Kwa mujibu wa IMF takribani fedha zaidi *$1 trillion* zilitengwa mahususi kama mpango wa dharula wa kuwezesha kifedha zaidi ya nchi 90 zilizoathirika na UVIKO-19. Mpaka sepemba 2021, IMF kupitia Rapid Credit Facility (RCF) na Rapid Financing Instrument (RFI) imeidhinisha mikopo kwa mataifa yanayoendelea kiuchumi. Hadi Juni 2021, nchi za EAC zimefaidika na mikopo hiyo; *Rwanda $111.06 ml, Uganda $1 bl, Kenya $739 Ml.*
Mh. Rais SSH anaichora ramani ya Tanzania tena kwenye uso wa dunia kwa uwezo wake kidiplomasia, sasa TUMEELEWEKA. Majadiliano na Mkurgenzi wa IMF Bi. Kristalina Georgieva, yamezaa matunda mkopo wa *$571 million* ili kujikwamua na madhara ya UVIKO.
Leo nikiwa katika uzinduzi wa kampeni ya maendeleo ya taifa ya miezi 9 ijayo, Nimesikiliza hotuba ya Rais, mwelekeo tunaouchukua KITAIFA, mpango, mgawanyo na mategemeo ya serikali kwa kiasi hicho *(Tsh. 1.3 Trillion),* imegusa mambo MUHIMU kwa msisitizo, *INFORMATIVE* and *DIRECTIVE* speech ever!
*i. Allocation* : Serikali ilivyoainisha vipaumbele, kugawa na kuelekeza fedha hiyo, imejikita kwenye VISABABISHI vya tatizo husika, vitendea kazi na miundombinu ya AFYA, ELIMU, na maji. Hii ni akili kubwa.
*ii.Usimamizi wa fedha* : kwa kuwa ni mpango wa miezi 9 tu, Rais amesisitiza zaidi na kuonya wanaofikiria kufuja fedha.
*iii. AMANI* :Jinsi Mh. Rais anavyotilia msisitizo swala la amani, Tanzania kuaminiwa na SADC kuongoza masuala ya amani ni chachu kwa maendeleo.
*NINASHAURI* 👇🏽;
*1* . Mh Rais, viatu vya Hayati JPM vinakutosha, sio vikubwa. Mafanikio uliyokwishayafikia kwa miezi 6 tu, iweje kwa kasi hiyo miaka 5 ijayo!.UNAWEZA !
*2* . *Usimamizi* : Miradi inakwenda kwa pamoja, ni vema VYOMBO vya usimamizi visiwe vingi zaidi, serikali ibane matumizi na mianya ya upigaji tupunguze kamati, POSHO, vikao nk, Ikiwezekana kiwepo CHOMBO kimoja tu. Watumishi waelewe nia njema ya Rais.
*3*. *Masharti nafuu* : fedha hizi sio GRANTS japo mi masharti nafuu, tulete unafuu kwa wananchi kwa kubana mianya ya upotevu wa fedha, na RUSHWA.
*4* .*AMANI* ; tuendelee na kuhakikisha kuwa Tanzania ni salama muda wote.
#VisitTanzania2021
No comments:
Post a Comment