Saturday, October 9, 2021

DKT MABULA: RAIS SAMIA ANAUPIGA MWINGI, ILEMELA TUMUUNGE MKONO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akihutubia wananchi wa kata ya Kayenze

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akipita kukagua shughuli za maendeleo katika Kisiwa Cha Bezi


Dkt Mabula ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi, kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kutoa mrejesho wa vikao vya bunge la bajeti na kushukuru wananchi kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu ulioisha mwaka jana eneo la Kisiwa Cha Bezi Kata ya Kayenze ambapo amesema kuwa zaidi ya Milioni 385 zimetolewa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ndani ya kata ya Kayenze, Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa kituo Cha afya Kayenze, Milioni 60 kwaajili ya ukamilishaji wa maabara mbili za shule ya sekondari Kayenze, Milioni 50 kwaajili ya Zahanati katika Kisiwa Cha Bezi, Milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya mtaa wa Bezi na Milioni 15 kwaajili ya shule ya msingi Kayenze

‘.. Kama Kuna watu wananufaika na jitihada za Rais Mhe Samia basi wana Ilemela mnatakiwa mmuombe na mumshukuru sana Mhe Rais, Fedha nyingi Sana zimekuja kwaajili ya Maendeleo ndani ya kata hata Jimbo ..’ Alisema

Aidha Mhe Dkt Mabula akawataka wananchi hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 sambamba na kuwasisitiza kujitokeza kwaajili ya chanjo Ili wasiweze kupata athari zaidi pindi wanapopata maambukizi ya ugonjwa huo kwani athari za ugonjwa kwa mtu aliyechanjwa ni tofauti na zile za mtu ambae hakupata chanjo.

Kwa upande wake Mhandisi Mndeme kutoka wakala wa Barabara za mijini na vijijini TARULA wilaya ya Ilemela mbali na kupongeza jitihada zilizofanywa na Mbunge huyo katika kuhakikisha bajeti inaongezeka mpaka kufikia bilioni tatu kitu ambacho hakijawahi kutokea hivyo kuwaasa kuendelea kushirikiana Ili miradi yote iliyokusudiwa iweze kukamilika

Nae Afisa Ardhi mteule wa Manispaa ya Ilemela Bi Biligita Msandya amewataka wananchi wa kata hiyo wanaodai fidia za ardhi kuwa wavumilivu kwani Serikali inaitambua changamoto hiyo na watakuwa wakilipa awamu Kwa awamu mpaka madeni yote ya fidia yatakapokwisha.

Moja ya mwananchi aliyehudhuria mkutano huo uliofanyika Kayenze senta Bi Joyce Desdudit amefafanua kuwa anaridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan sanjari na kuwaomba kuungana pamoja kuhakikisha nchi inasonga mbele.

No comments:

Post a Comment