Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa zao la ndizi
Kanda ya Kaskazini uliofanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, leo Septemba 25, 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo)
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kilimanjaro
WAZIRI wa Kilimo, Mhe Prof. Adolf Mkenda, amewataka wadau wa zao
la ndizi nchini ikiwemo wawekezaji kuchangamkia frusa ya kuzalisha kwa wingi
zao hilo ambalo kwa sasa limewekewa mkakati wa kuwa zao kubwa la kibiashara.
Profesa Mkenda ameyasema hayo Leo tarehe 25 Septemba 2021 mjini
Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua mkutano wa wadau wa zao hilo Kanda ya
kaskazini ambapo amesema pamoja na wizara hiyo kuthamini na kuyapa kipaumbele
mazao mengini lakini pia ndizi ni zao muhimu kibiashara.
Amesema serikali ipo tayari kuwaunga mkono wadau wote ikiwemo wa
uwekezaji na wakulima wakubwa wa zao hilo kutokana na kwamba wizara ya
Kilimo imelipa umuhimu mkubwa kwa lengo la kuwa zao la kibiashara.
Amesema kuwa, katika nchi nyingine zao hilo limekuwa
likizalishwa kwa wingi ambapo kwa mwaka huzalishwa kwa Tani elfu 60 hadi 70 na
kuuzwa maeneo mbalimbali Duniani na kuzinufaisha nchi hizo kiuchumi na kwamba
wawekezaji wanapaswa kuona fursa hiyo.
"Zao la ndizi ni muhimu kama zao la chakula na Kama matunda lakini kwa namna tunavyo shughulika na kilimo hichi ni tofauti na nchi nyingine ambapo hulilima kama zao la biashara hivyo naombeni wadau mchangamkie frusa hii kwani serikali ina mkakati wa kuhakikisha zao hili linakuwa la biashara" Amesema Profesa Mkenda
Aidha, amesema katika kuhakikisha zao hilo linazalishwa kwa tija, serikali itahakikisha inaongeza na kuboresha huduma za ugani ikiwa ni pamoja upatikanaji wa mbegu bora kwa kushirikiana na wadau.
"Serikali ipo na tutahakikisha tunashirikiana na wadau wote kwa kufanya kazi nanyi bega kwa bega na naomba tushikamane wote tuendeleze zao hili kama ilivyo kwa mazao mengine" Amesema Mkenda
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, ameziagiza Halmashauri za wilaya nchini kujenga vituo vya ukusanyaji wa zao hilo kwa kuwawezesha vijana kwa kuwakopesha asilimia 10 ya mapato inayotengwa.
Amesema kuwa (TAMISEMI) inaunga mkono jitihada zinazofanywa na
wadau wake katika kuhakikisha watanzania wananufaika na zao hilo pamoja na
mazao mengine na kwamba serikali wamekuja na mpango wa kuhakikisha wakulima wa
ndizi wanaongeza thamani ya ndizi.
Naye Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya mbogamboga, Maua na matunda(TAHA), Dkt Jackline Mkindi amesema kuwa lengo la kuwakutanisha wadau hao ni kwa ajili ya kuaandaa mkakati wa pamoja wa kufufua zao la ndizi kitaifa na kimataifa ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya zao hilo na kuongeza mnyororo wa thamani.
MWISHO
No comments:
Post a Comment