Sunday, September 26, 2021

WAZIRI MKENDA AONGOZA HARAMBEE UJENZI WA MSIKITI WA KAUTHAR TARAKEA WILAYANI ROMBO

Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo mbele ya waumini ya Dini ya Kiisalamu Wilayani Rombo katika harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea, Leo tarehe 26 Septemba 2021. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo mbele ya waumini ya Dini ya Kiisalamu Wilayani Rombo katika harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea, Leo tarehe 26 Septemba 2021.
Sehemu ya waumini wa kiisalmu wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi-Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda  kabla ya harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea, Leo tarehe 26 Septemba 2021.
Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Rombo Shekh Abdallah Bakari Mbago akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi-Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda  kabla ya harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea, Leo tarehe 26 Septemba 2021.
Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo mbele ya waumini ya Dini ya Kiisalamu Wilayani Rombo katika harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea, Leo tarehe 26 Septemba 2021.

Na Mathias Canal, Kilimanjaro

Mbunge wa Jimbo la Rombo ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Prof. Adolf Mkenda leo tarehe 26 Septemba 2021 ameongoza waumini ya Dini ya Kiisalamu Wilayani Rombo katika harambee ya kupunguza deni la ujenzi wa msikiti wa Kauthar Tarakea ambapo jumla ya Shilingi 21,833,500 zimepatikana.

Msikiti huo ambao umekamilika Ujenzi wake kwa kiasi kikubwa umegharimu fedha za kitanzania Tsh 486,547,635 kwa kutolewa na wafadhili mbalimbali wa ndani na nje ya Wilaya ya Rombo ambao ni waislamu na wasiokuwa waislamu.

Katika fedha hizo za ujunzi jumla ya kiasi cha Shilingi 33,443,600 zinadaiwa baada ya ujenzi huo kukamilika hivyo harambee hiyo ni sehemu ya kulipa deni hilo.

Imeelezwa kuwa fedha zilizokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali ni jumla ya Shilingi 453,114,035 hivyo kuwa na deni ambalo linahitaji kukamilishwa.

Katika mkutano huo Waziri Mkenda amehimiza Upendo, Amani na Mshikamano kwa waumini wote wa kiislamu pamoja na wale wasiokuwa waislamu kwani kufanya hivyo kutaimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla wake.

Waziri Mkenda amesema kuwa viongozi wa dini pamoja na waumini wote wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania ili liendelee kuwa na Amani ambapo amesisitiza umuhimu wa kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwani kazi ya kuongoza nchi ni kubwa na inahitaji maombi na ushirikiano wa watanzania wote.

Awali, akisoma risala wakati wa harambee ya fedha za kulipa deni la ujenzi wa msikiti, Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Rombo Shekh Abdallah Bakari Mbago amesema kuwa ujenzi wa msikiti huo kuwa wa ghorofa ulitokana na ongezeko la waislamu mwaka 2010.

Pamoja na mambo mengine Shekh Bakari amemshukuru Waziri wa Kilimo Prof Adolf Mkenda kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuendesha harambee ya msikiti huo. “Tunakushuru sana Mhe Waziri kwa kuendesha harambee hii, nakuhakikishia tangu tuanze kufanya harambee katika wilaya ya Rombo hatujawahi kupata kiasi kinachozidi Mili ishirini wewe umetuvunjia mwiko” Amesisitiza

MWISHO

No comments:

Post a Comment