Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameliagiza jeshi la polisi wilaya ya Iringa akijaribu kuwasaka waharifu wanaohusika katika tukio la uchomaji moto nyumba ya mwenyekiti wa kijiji cha Lumuli
wananchi wakiwa makini kumsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa wakati wa ziara yake katika tarafa ya Kiponzero
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ameliagiza jeshi la polisi wilaya ya Iringa kusakwa na kutiwa mbaroni watuhumiwa wote wanashukiwa kuiteketeza kwa moto nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji Cha Lumuli
Akizungumza katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho cha Lumuli,Moyo amelitaja tukio hilo ni la kikatiri na halipaswi kufumbiwa macho kwa kuwa limehatarisha uhai wa kiongozi huyo wa Serikali.
Moyo alisema kuwa haiwekani wananchi wakajichukulia sheria mkononi kwa kutaka kumzuru kiongozi wa kijiji hicho kisa tu amekuwa na msimamo wa dhati kuhakikisha shughuli za kimaendeleo zinachangiwa na wananchi wote.
Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan analeta fedha kwa ajili ya kuchochea kuleta maendeleo ya kijiji lakini wananchi wachache wanaamua kukwamisha kwa makusudi jambo hilo halikubariki hata mara moja.
Aidha Moyo kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Mkutano huo Watu wasiofahamika wanadaiwa mnamo wiki mbili zilizopita walivamia na kuiteketeza kwa moto nyumba ya mwenyekiti wa Kijiji hicho huku chanzo Cha tukio Hilo ikielezwa ni chuki zilizotokana na baadhi ya wanakijiji kupinga shinikizo la kushiriki shughuli za maendeleo Kijijini hapo.
Alisema kuwa atahakikisha watu wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa katiba ya nchi inayosema kwa watuhimiwa wa makosa ya namna hiyo.
Moyo alimtaka mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Iringa kuhakikisha wanawapata wote waliohusika na tukio hilo kisha kuwapeleka mahakani haraka iwekavyo ili iwe funzo kwa wananchi wangine wenye nia kama hiyo.
Alisema jukumu la kufanya shughuli za kimaendeleo katika kijiji ni jukumu la wananchi wa kijiji husika hivyo ikitokea kama kuna mtu anakaidi kuchangia shughuli za kimaendeleo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa upande wa diwani wa kata ya Lumuli Yohanes Mlusi alisema kuwa wananchi walichoma nyumba ya mwenyekiti Mendrad Nywage ni chuki za kisiasa tu ndio zimechangia tatizo hilo kwa kuwa amekuwa na msimamo wa kusimamia vilivyo sheria za kijiji kwa lengo la kusaidia wananchi kupata maendeleo.
Alisema kuwa mwenyekiti huyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kukuza uchumi wa wananchi na kusimamia vizuri miradi ya kimaendeleo ambayo inakuwa inatekelezwa katika kijiji hicho.
Alisema kuwa wananchi ambao wamekuwa hawataki kusaidia kuchangia shughuli za maendeleo katika kijiji hicho ndio wamekuwa wanamchukia mwenyekiti wa kijiji hicho kwa msimamo wake wa kuhakikisha wananchi wote wanashiriki kwenye maendeleo ya kijiji hicho.
Lakini pia diwani huyo Mlusi alisema kuwa licha ya kuwa kuna chuki ya kisiasa kumekuwa na kutoelewana kwa afamilia yake mara baada ya kuachana na mke wake wa kwanza mwenye watoto wakubwa kiasi kwamba baadhi ya wananchi wanahisi kuwa vitu vyote vinavyomtokea kiongozi huyo vinafanywa na familia ya mke mkubwa.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Iringa OCD Maganga Ngosha,mkuu wa kituo cha polisi cha Ifunda kinachohudumia tarafa ya Kiponzelo kilicho katika kijiji cha Ifunda Agustino Marema alisema kuwa wameshaanza kulifanyia kazi tukio hilo na tayari wameshawakata baadhi ya wananchi wanaosadikika kuwa wanahusika na tukio la kuchoma moto nyumba hiyo ya mwenyekiti.
Alisema kuwa baada ya kupata taarifa la tukio hilo wachukua hatua mara moja ya kuanza kuwatafuta wahusika wote na kuongeza namna ya kufanya upelelezi ili kuwabaini waarifu wote waliofanya kitendo hicho cha kuchoma nyumba hiyo ya mwenyekiti.
Aliwataka wananchi wote wa tarafa ya Kiponzero kushiriki katika ulinzi shirikishi ili kupunguza na kuyaondoa matendo yote ya kiharifu ambayo yamekuwa yanavuruga amani ya wananchi ambao sio waharifu na wapenda maendeleo.
No comments:
Post a Comment