Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akisaini kitabu cha wageni katika Gereza Kuu la Wanawake, Mkono wa Mara, Kingolwira Mkoani Morogoro alipofanya ziara Gerezani hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu akizungumza na Maafisa Magereza alipofanya ziara katika Gereza Kuu la Wanawake, Mkono wa Mara, Kingolwira Mkoani Morogoro.
Na Mwandishi Wetu Morogoro
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. John Jingu ametembelea Gereza Kuu la Wanawake la Mkono wa Mara, Kingolwira Mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa ustawi na wanawake, Watoto na wazee wanaotumikia adhabu ya kifungo katika magereza mbalimbali nchini.
DKt. Jingu amesema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuwawezesha wataalam hao kutafuta ufumbuzi changamoto za jamii wakiwa na uelewa mpana kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hasa makundi hayo maalum.
Aidha amesema kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inajumuisha masuala yote yanayohusu wanawake, wazee na watoto kwahiyo ni muhimu kutafuta suluhisho la matatizo kwa watanzania wote bila ubaguzi na hivyo kuamua kufanya ziara katika magereza mbalimbali kuwasalimia na kuwasikiliza wafungwa.
“Sisi tunashughulikia masuala yote ya Maendeleo ya Jamii wakiweno hawa waliko magerezani tukiwatembelea na kuwasikiliza tutakuwa katika nafasi nzuri ya kutafuta suluhisho la matatizo ya kijamii”alisema Dkt. Jingu.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Gereza hilo Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Flora Mbalawa ameipongeza Wizara kwa hatua ya kufanya ziara na kusikiliza maoni na mapendekezo ya watumishi na wafungwa ili kutafuta namna bora ya kutatua changamoto za jamii.
No comments:
Post a Comment