Naibu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme, leo
amezindua kampeni za ubunge jimbo la Ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga.
Mndeme,
amesema mgombea huyo Emanuel Peter Cherehani, anatosha kurithi viatu vya
aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ambaye pia alikuwa Waziri wa Ulinzi, marehemu
Elias Kwandikwa.
Uzinduzi
wa kampeni hizo umefanyika katika viwanja vya Nyamilangano, ambapo CCM kimetumia
fursa hiyo kumsimamisha Ndugu Emmanuel Peter Cherehani na kumkabidhi Ilani ya
Uchaguzi ya 2020/2025 ya Chama hicho.
Katika
hatua hiyo, Mndeme alisisitiza kuwa Chererehani ana uzoefu wa uongozi katika
kutetea maslahi ya wananchi wa Ushetu, hususani katika masuala ya kilimo,
elimu, afya na maboresho ya miundombinu.
Aliongeza
kuwa, mgombea huyo amekuwa Mwenyekiti wa vyama mbalimbali vya ushirika ikiwemo
cha wakulima wa Tumbaku,Chama cha Mwadui na Ubangwa na mtetezi wa maendeleo ya
wakulima wa pamba.
Katika mkutano huo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walihudhuria akiwemo Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Ndugu Maudline Castiko, wabunge wa mkoa wa Shinyanga na mamia ya wananchi.
No comments:
Post a Comment