Waziri wa Nchi OR- TAMISeMI Mhe. Ummy Mwalimu akitoa pongezi kwa Uongozi wa Manispaa ya Kahama baada ya akifungua nyumba za Walimu (6 in 1) zilizojengwa katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu akifungua nyumba za Walimu (6 in 1) zilizojengwa katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Philemon Sengati
Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na hadhara wakati wa hafla ya kufungua nyumba za Walimu (6 in 1) zilizojengwa katika Shule ya Msingi Magobeko Kata ta Kinaga kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kahama. Muonekano wa Nyumba za Walimu ( 6 in 1) zilizofunguliwa na Waziri wa Nchi OR- TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ziara yake kwenye Manispaa ya Kahama.
*************************
Nteghenjwa Hosseah, Kahama
Wahenga husema usiibe kabla Jua halijazama,pengine ndio kauli inayofaa kusemwa kwa Wananchi wa Kata ya Kinaga iliyopo pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katikati ya kukata tamaa kusikoelezeka kwa wananchi wa Kata ya Kinaga wanaofikia idadi ya Elfu kumi na sita (16,000)kwa mujibu wa Taarifa za Manispaa ya Kahama,Uzinduzi wa Nyumba sita za Walimu uliofanywa na Waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu unaleta Ahueni ya kipekee kwao.
“Hongereni sana kwa Juhudi za kujenga kuboresha Miundombinu ya Kusomea watoto wetu mnazofanya ni Matumaini yangu kuwa Nyumba hizi tunazozindua leo kwaajili ya Walimu wetu zitachochea Ufaulu wa watoto wetu kwakuwa sasa Walimu watafundisha pasipo adha ya kuwaza Makazi”Amesema Ummy Mwalimu Waziri wa Tamisemi.
Baadae Waziri Ummy akamuagiza Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Dk. Grace Maghembe Kuingiza Kata ya Kinaga kwenye orodha ya Kata za Kimkakati ili iweze kupatiwa fedha za Ujenzi wa Kituo cha Afya kitakachosaidia Akinamama Wajawazito kujifungua salama pasipo vikwazo.
Pamoja na Ahueni ya Kujengewa kituo cha Afya lakini pia Waziri Ummy amemuelekeza Katibu Mkuu Tamisemi,Prof. Rizik Shemdoe kuwaagiza Tarura kuijenga barabara ya Magobeko kwakiwango cha Changarawe ili iweze kupitika wakati wote.
Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philmon Sengati amesema Mkoa huo utendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya Kimaendeleo ikiwemo kusogeza karibu Huduma za Afya na kuboresha Miundombinu ya Barabara.
Kata ya Kinaga Katika Manispaa ya Kahama ndio kata iliyopo pembezoni kuliko ikiwa na umbali wa Km 22 kutoka Makao Makuu ya Halmashauro ya Kahama.
No comments:
Post a Comment