Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Kongwa
Waziri
wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) jana tarehe 17 Agosti 2021 amemkabidhi
zawadi ya Televisheni Afisa Ugani Kata ya Ng'humbi Ndg Charles Mujule kama kielelezo cha kutambua
utekelezaji wa kazi yake.
Waziri Mkenda ametoa
zawadi hiyo wakati wa kikao kazi alipokutana na kuzungumza na maafisa ugani wa
Wilaya ya Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri
ya wilaya ya Kongwa.
Amesema
kuwa maafisa ugani ndio mboni ya jicho la Wizara ya Kilimo hivyo ili nchi iweze
kuwa na kilimo bora kinachokidhi matakwa ya tija na wingi wa uzalishaji na kuwa
na kilimo kitakachokidhi matakwa ya soko ni wazi kuwa elimu ni muhimu itolewe
kwa wakulima.
Waziri
wa Kilimo amesisitiza kuwa bila kufanya kazi kwa ufanisi na maafisa ugani
kilimo hakiwezi kupiga hatua za kimaendeleo hivyo serikali imekuja na mkakati
wa kuwatambua na kuwapa mashamba ili wawe mfano kwenye sekta ya kilimo.
Akizungumza katika
mkutano huo mara baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo awfisa Ugani wa Kata ya
Ng'humbi Ndg Charles Mujule amemshukuru Waziri Mkenda kwa kutambua na kuthamini
kazi kubwa zinazofanywa na maafisa ugani nchini.
MWISHO
No comments:
Post a Comment