Thursday, August 5, 2021

WADAU IBUNGILO WAPONGEZWA USHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO

 

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masala akikagua ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Ibungilo

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla akizungumza na walimu wa shule ya sekondari Ibungilo alipotoa fursa ya kuwasilisha kero zao

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Kiloleli kata ya Ibungilo

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hassan Elias Masalla akikagua ujenzi wa soko la kiloleli kata ya Ibungilo

Wadau wa maendeleo wamepongezwa na kuombwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kupunguza adha kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Hasan Elias Masalla wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ibungilo katika viwanja vya soko la Kiloleli ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo, kujitambulisha kwa wananchi, kuwakumbusha wananchi juu ya uchukuaji wa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili akiwa na wataalamu wa manispaa ya Ilemela  ambapo amewashukuru wadau wanaounga mkono shughuli za kimaendeleo kwa kuchangia kwa hiari nguvu na mali katika utekelezaji wa miradi inayosaidia kupunguza changamoto zinazoikabili jamii

‘.. Kwakweli nawapongeza sana watu wa Ibungilo, Nmeona nguvu za wadau na wananchi kwa ujumla, Nmeona thamani ya fedha katika ujenzi wa maabara, Nmeona ushiriki wa wadau katika maendeleo ya soko letu ..’ Alisema

Aidha Mhe Masalla akawaahidi wananchi hao kuwa atakaa na viongozi wa soko la Kiloleli, watalaam wa manispaa katika kutatua kero za soko hilo huku akiwaasa kuendelea kumuombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na Serikali anayoiongoza ili waweze kuwatumikia kwa uadirifu na kuwaletea maendeleo

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela ambae pia ni afisa ardhi na mipango miji Ndugu Shukran Kyando mbali na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na mkuu huyo wa wilaya, Akawataka wananchi hao kuheshimu sheria za ardhi na mipango miji kwa kuhakikisha wanajenga kwa kufuata sheria ikiwemo kuwa na vibali vya ujenzi sambamba na kuongeza kuwa Serikali haitamvumilia mtu yeyote atakaefanya maendelezo ya ardhi bila kufuata sheria na taratibu ikiwemo kuvunja nyumba zitakazojengwa kiholela na faini ya hadi laki saba kwa atakaeng’oa vigingi vya mipaka ya ardhi.

Nae Diwani wa kata ya Ibungilo Mhe Husein Magela akamshukuru mkuu huyo wa wilaya huku akiahidi kuendelea kushirikiana nae katika kuwatumikia wananchi wa kata hiyo na kuwaletea maendeleo

Kalala Magafu ni mjasiriamali katika soko la Kiloleli kata ya Ibungilo ambapo kupitia mkutano huo wa mkuu wa wilaya ya Ilemela  amelalamikia viongozi wa soko hilo kutumia mamlaka yao vibaya kwa kunyanyasa wafanyabiashara wadogo na kujinufaisha wao binafsi hoja ambayo ilipokelewa na kuahidi kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment