Na Fredy Mgunda,Iringa.
MWENGE wa Uhuru umepongeza
miradi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa kutokana na kuwa na ubora unaolingana
na thamani ya miradi na kusaidia kuchochoe maendeleo kwa wananchi wanaokusudiwa
katika kukuza uchumi wan chi.
Akizungumza wakati wa
kutembelea na kugagua miradi hiyo mkimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa Luteni
Josephine Mwampashi Alisema
kuwa wameridhishwa na miradi waliyoitembelea wakati wa mwenge wa Uhuru
ulipokuwa katika Halmashauri hiyo.
Mwampashi alisema kuwa
wamejionea mradi mzuri wa wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa kupambana na rushwa
unaotekelezwa katika shule ya sekondari ya Nyerere iliyopo katika Halmashauri
ya wilaya ya Iringa ambao unalenga moja kwa moja kuendelea na mapambano dhidi
ya rushwa kuanzia shuleni.
Alisema kuwa kwa sasa kuna
vijana wengi ambao wanatakiwa kuendelea kupata elimu ya kupambana na rushwa ili
hapo baadae kuwe na kizazi ambacho kitakuwa kinajua madhara ya kupokea au kutoa
rushwa.
Katika hatua nyingine kiongozi
huyo Mwampashi alisema kuwa mradi wa kilimo uliopo katika kijiji cha Kising’a
umekuwa mradi bora kati ya miradi ya mwenge ambayo imetembelea kwa kuwa
unamanufaa makubwa kwa wananchi wanaouzunguka mradi huo na wale waliopo nje ya
mradi huo.
Alisema kuwa wananchi wa
Halmashauri ya wilaya ya Iringa wanatakiwa kula mlo kamili ili kupunguza na
kuondoa kabisa tatizo la utapiamlo na udumavu kwa watoto wadogo kwa kuwa
wanaardhi ambayo inafaa kwa kilimo cha aina yoyote ile.
Awali akisoma taarifa ya mradi
wa kilimo cha mboga mboga na matunda katika kijiji cha kising’a ,afisa ugani wa
kata ya kising’a Stanley Mwengilolo alisema kuwa mradi huo umegharimu kiasi cha
shilingi 87,705,000 ambacho ndio kinatekeleza mradi huo mkubwa wenye manufaa
makubwa kwa wananchi wa kata hiyo na nje ya kata hiyo.
Mwingilolo alisema kuwa mradi huo
kwa kiasi kikubwa umefanikishwa na uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa
kuanzia ngazi ya awali hadi ulipo fika kwa lengo la kuchochea maendeleo katika
sekta ya kilimo.
Alisema kuwa mradi huo umekuwa mfano wa kuigwa kwa wananchi wote wanaopenda kilimo cha mboga mboga na matunda kwa kulima kilimo cha kisasa ambacho kimekuwa na faida kwa wananchi wanaolima kilimo hicho.
No comments:
Post a Comment