Friday, August 20, 2021

MATUKIO KATIKA PICHA KIKAO CHA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII NA WIZARA YA HABARI

Viongozi Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakijadiliana kabla ya kuingia kwenye kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuwasilisha taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Mpira wa Miguu na Bodi ya Ligi katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, leo Agosti 20,2021.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa akiwasilisha taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Agosti 20,2021.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Stanslaus Nyongo akiongoza kikao chake cha kupokea  taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Mpira wa Miguu na Bodi ya Ligi katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma, leo Agosti 20,2021.

Viongozi Wakuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakichukua maoni kutoka kwa wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii walipokuwa wakichangia  taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT)  wakati wa kikao cha  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Agosti 20,2021.

No comments:

Post a Comment